![Walete ft. Aslay](https://source.boomplaymusic.com/group10/M00/11/26/466e8903bff7465ab9aa6182882bee2b_464_464.jpg)
Walete ft. Aslay Lyrics
- Genre:Hip Hop & Rap
- Year of Release:2021
Lyrics
Walete ft. Aslay - Stamina (TZ)
...
ASLAY. mhhh yee yeee oaaaah
STAMINA
(wamemchokoza Bea)
alieleta hili galika lamapenzi hana msaada
ukiona rohoyako inasita ongeza moja ziwe saba
wenye myoyo mikubwa wako kwa machela
wenye myoyo midogo ndo daily vifo mwaisela
kwani niyupi anaekupenda toka moyoni
halafu ukimcheki usoni macho yote yako mfukoni
na niyupi atayefanya uende motoni
ushamshika hadi ugoni bado unampenda hukomi
salamu brother adam kwanini ulikula tunda
bora ungemla hawatusingekuwa mapunda
onasasa mapenziyakweli hatuyajui
tunaishi kama kondoo kwenye zizi moja na chui
unaweza usimtake wamasaki kisa unahela kidogo
ukampata wa mbulahati na ukaibiwa na kigogo
yani mapenzi bwana yanauongo wa ku pretend
unaweza ukachunwa nahuri nabado ukaonyeshwa stend aisee
ASLAY
waleeete kwangu mi mshauli wamapenzi
wagonjwa lilete Mungu baba aah
wasameehe waliotesa watu kisapenzi
niwaombee kwako Mungubaba wasameehe
STAMINA
unateseka na mapenzi mwaka wa kumi sasa
moyowako mlango kila unaempa anavunja kitasa
kunamuda unajiona ka unapitwa na wakati
mpaka supu ya pweza unainywa na chapati
wangapi wanapenda shape kwa msichana asie na akili
huku mwenye akili shape kwake so dili
ukimtaka mcha Mungu Mungu anakupa mdangaji
ilachaajabu huyomdangaji ndo anakupa unavyohitaji
neno MA inaanisha hakunampenzi zaidi ya mama
PE peleka posa paleunapozama
NZI hakikisha basi unamuenzi milele
hata akikucheat useme yalopita si ndwele
unaempenda kisamacho sikuya ukipofu itakuwaje
unaempenda kisamwendo Siku ya ukiwete itakuwaje
mwenye maneno matamu ukiwa kiziwi utamsikiaje
dah hayamambo bwana tutafanyaje
ASLAY
waleete kwangu mi mshauli wa mapenzi
wagonjwa liletee Mungu baba aah
wasamehe waliotesa watu kisapenzi
niwaombee kwako Mungu baba wasamehe
roho juu juu mapenzi kilema yani upofu tu
hayana madogo yanamakuu uwenagari au kwa miguu
utaumia eeh
yalimfanya babu akamwacha bibi
yalimfanya juma ajione p Didy
yalinifanya mi njione zaidi
nikahama temeke
walete kwangu mi mshauli wa mapenzi
wagonjwa liletee Mungu baba (ah)
wasameehe waliotesa watu kisapenzi
niwaombee kwako Mungu baba wasameehe
(wamemchokoza Bea)