Machozi ft. Bushoke Lyrics
- Genre:Hip Hop & Rap
- Year of Release:2023
Lyrics
Machozi ft. Bushoke - Stamina Shorwebwenzi
...
Ooi
niaje mwamba samahani nakusumbua
Naomba usikate simu taratibu utanijua
Nampigia mke wangu naona hapokei simu
Ila najua umelala nae sorry nakukata stimu
Na unanijua, na unajua si ni wazazi
Naumia kuona wanangu wanalala na dada wa kazi
Na usiulize namba yako nimeitoa wapi
Naomba uskize mi mumewe wa ndoana sio mchat
Kwanza nikupe pongezi we mjasiri
Mi kulala na mke wa mtu siwezi
Unapata nguvu ipi kujipa hayo mamlaka
Angali mme wake yu hai hajafa hajampa talaka
Halafu
Naskia unasound umechoka sana
Ndo mshamaliza round ya kwanza au sio mwana?
Wakati mimi nalalia mito
We unaenjoy tu unamkunja kama kiko
Vp mtamu eeh!? Kanona eeh?!
Nagharamika bro sijui kama unanisoma aisee
Najua unampenda sababu unamhudumia
Nataka nikuachie bro uone jinsi navyoumia
Kama kidume cha mbegu kesho nkuletee watoto
Uwalee na mke wangu unipunguzie msoto
Inaniuma nimehudumia nimempa thamani
Zamani nakuhakikishia ungemwona usinge mtamani
Kama anasema ndoa imekufa daah changamoto
Au anasema tumeachana nimebaki nalea watoto
Sorry salio linakata naweka vocha nakupigia
Ili unipe simu niongee na huyo mshenzi wa tabia.
Chorus
Kama binadamu una moyo sio chuma naumiaaa
Machozi yanitoka nashindwa vumiliaaa
Natamani niondoke hata kwenye hii duniaaaa
Mana heshima yangu we uneshindwa nitunziaaaa
Wananiumiza moyo, akili yangu haisomi
Umenishusha thamaniiii
Nadharaulika mtaaniiiii
Verse 2
Halloo
Pole sana kwa uchovu
Pole kwa kazi nzito ya kubeba pembe ya ndovu
Najua ulipanga unidanganye boya lako
Kuwa party iliisha late ukalala kwa shost yako
Kukuita malaya sitaweza
Umenizalia watoto ila heshima unaipoteza
Japo mambo unayofanya ya kiasherati we sio smart
Umesahau unafamilia au na watoto huwataki
Okay Tuseme skuridhishi kitandani
Je anaetoa kodi ya meza hapa nyumbani ni nani?
Unadhani watoto watakula tu sex eti
Au nkikosa hela watalishwa na bwana yesu
Zile makeups, kusuka, wanja, saloon ungezipata wapi nisingekaza kisabuni
Hata kama sio handsome nilitimiza majukumu
Sa huyo atakupa nini zaidi ya kukulisha ndumu
Wazazi waliposema kuwa tukapime DNA
Nilisema wamezeeka hawa wazazi TZA
sasa hivi naelewa kila nikiwacheki watoto
Sura yangu inakuja inaondoka changamoto
Ukirudi nyumbani chukua kilicho chako
Tena ikibidi nenda na watoto wako
Nauonea huruma huo mfuko wako wa uzazi
Ungekuwa mfuko wa kawaida ningesha ubebea viazi.
Chorus
Kama binadamu una moyo sio chuma naumiaaa
Machozi yanitoka nashindwa vumiliaaa
Natamani niondoke hata kwenye hii duniaaaa
Mana heshima yangu we uneshindwa nitunziaaaa
Wananiumiza moyo, akili yangu haisomi
Umenishusha thamaniiii
Nadharaulika mtaaniiiii
Oscar Chilunda
0735512554
23/2/2023