![Hakuna Kama Wewe ft. Walter Chilambo](https://source.boomplaymusic.com/group10/M00/11/26/466e8903bff7465ab9aa6182882bee2b_464_464.jpg)
Hakuna Kama Wewe ft. Walter Chilambo Lyrics
- Genre:Hip Hop & Rap
- Year of Release:2021
Lyrics
Hakuna Kama Wewe ft. Walter Chilambo - Stamina (TZ)
...
Aaaaaaaa Aaaaaaaa
STAMINA
Nikipata kiu Baba, ninyweshe maji ya baraka.
Nikipata njaa nilishe sakriment iliyotakaswa
Gusa baba, maisha yangu yaguse ikibidi nipe fimbo ile ya Musa inivushe
wangap walisema kua sitokwenda popote chaajabu hapa nilipo wanataman tuwe wote
Na wengine walisema kua sina lolote,
Chaajabu leo wanaomba niwasaidie chochote
Nishapigwa Vita vingi vya mikuki na mishale
ila sianguki kwao naanguka mbele ya ilkare
Haikua rahisi kufika si mchezo nahitaji pongezi nyingi za Ubani chetezi
Mungu wa Mganga ni Wewe (wewe)
Wa mwizi ni Wewe (wewe)
Wa mchawi ni wewe
Wa kila mtu ni wewe (kila mtu ni wewe)
Hakuna kama wewe zaidi ya wewe mwenyewe,
Hata hiyo miungu mingine na yenyewe inakuomba wewe
Hakuna kama wewe baba (Usiyechagua)
Hakuna ila ni wewe tu (Nina kuamini Mungu baba)
Hakuna kama wewe baba (Baba wa upendo)
Hakuna ila ni wewe tu (Oooh.......)
Nikupe nini Bwana, Mana ninavyomba vyote unanjibu
Hata hadija akikopa unamlipa kwa utaratibu
Mimi ni nani mbele yako mpaka nishindwe kushukuru.
Unanipa pumzi ya bure bila kuilipia ushuru
Usinitoe kwa damu yako takatifu wa Roma,
Bali niokoe kwa hii vita Gomora na sodoma.
We ni Afla baba, tena Alfa na Omega Japo siku moja moja kanisani hua natega
Unapoona napotea Ona unanikumbusha misa, kama haitoshi umeweka msikiti na kanisa,
Na sio shekhe tu umenipa na katekista, Baba unatenda haki, Haki sawa Nama Sister
Bila wewe sizani kama ningejua Biblia,
wala Msaafu sizani ningeusujudia
Sina cha kukulipa japokua Haukopeshi
Hata ukinikopesha siwezi kulipa kwa Kesh
Mungu wa Mganga ni Wewe (wewe)
Wa mwizi ni Wewe (wewe)
Wa mchawi ni wewe
Wa kila mtu ni wewe (kila mtu ni wewe)
Hakuna kama wewe zaidi ya wewe mwenyewe,
Hata hiyo miungu mingine na yenyewe inakuomba wewe
Hakuna kama wewe baba (Mtetezi wa mnyonge)
Hakuna ila ni wewe tu (Usiyebadilika baba)
Hakuna kama wewe baba (Hakuna kama wewe)
Hakuna ila ni wewe tu (Hakuna kama wewe)
Hakuna kama wewe baba (Unayetoa kibali)
Hakuna ila ni wewe tu (wewe Unayeponya baba)
Hakuna kama wewe baba (Unanishindia vita yangu)
Hakuna ila ni wewe tu...
Mungu wa Mganga ni Wewe
Wa mwizi ni Wewe
Wa mchawi ni wewe
Wa kila mtu ni wewe
Hakuna kama wewe zaidi ya wewe mwenyewe,
Hata hiyo miungu mingine na yenyewe inakuomba wewe
Thank you.....