Ukizaliwa ft. Banana Zorro Lyrics
- Genre:Hip Hop & Rap
- Year of Release:2022
Lyrics
Ukizaliwa ft. Banana Zorro - Stamina (TZ)
...
Najua husikii ninayokwambia
Ila ukizaliwa nitarudia
Naomba uyatii ninatokwambia
Maana yadunia yanavutia
Kwahiyo ukizaliwa mama, ukizaliwa mamax2
Mama yako aliposema anamimba aliniboa, sikuwaza chochote zaidi yakumwambia toa.
Nisamehe maana kama nilipagawa, nilijiuliza tu hitakuwaje na kiuchumi sipo sawa.
Kumbe mungu, amekuleta kama baraka,hata ningekuwa ibrahim nisingekuta kama issiaka.
Acha na mimi mshukulu sana mama yako, kukubeba meizi 9 ningewezaje mimi baba yako.
Ukizaliwa kidume jua umeumbiwa mateso, utatimuliwa vumbi na husipewe hata leso, kuna muda wa dhiki kuna muda wa raha unaweza ukalala njaa na jirani akalala bar.
Kidume changu cha nguvu nitasubili tu ubalee, kuwaona wakwe zangu hiyo kwangu ni starehe,kosea vyote maishani ila husikosee kuoa,bola ukosee kujenga nyumba unaweza ukaibomoa.
Alafu mwanaume ni kuwa na chako sasa penda vyawenzako uone unavyotokwa jasho, macho mawili ndo kipimo cha ulijali, ukitoa jicho la tatu vitu utaviona kwa mbaali.
Ukiwa Kilema sawa, njiti. Sawa, hujafa hujaumbika mbona fiti sawa.
Mungu katuumba sawa sisi wote binadamu, ninachojua mimi kitanda hakizai haramu.
Najua husikii ninayokwambia
Ila ukizaliwa nitarudia
Naomba uyatii ninatokwambia
Maana yadunia yanavutia
Kwahiyo ukizaliwa mama, ukizaliwa mamax2
Ukizaliwa mwanamke kweli nitafurahi sana,hata jina nitakupa la marehemu mama,ila tabia naomba ufwate za mama yako husije ukatoa mimba endapo utapata kijacho.
Ukikua naomba ujitunze unanielewa,tambua wewe sio mdori husikubali kuchezewa,tafuta hela kichaga pesa mbele ukivunja ungo husiwape wapete mchele.
Mwanangu wanaume wenye pesa ni wengi,ila wenye mapenzi wapo wachache kishenzi, hapo akili kumkichwa mi ninachotaka posa, maana muaminifu hata mwamposa utamkosa eee.
Na ukiwa mchafu hata husije ukapagawa,maana mama yako mwenyewe atakufanyia baby shower, sitaki kabisa uwe mwanamke wa mwanamke nataka uwe mwanamke wa mwanaume uitwe mke.
Nitakopa hata vikoba usome husinyanyasike, mtaani kuwa na heshima baba yako husiniaibishe, mambo mengine ya dunia yakupite we wakike ukipata shida sema itatulike.
Ukiwa Kilema sawa, njiti. Sawa, hujafa hujaumbika mbona fiti sawa.
Mungu katuumba sawa sisi wote binadamu, ninachojua mimi kitanda hakizai haramu.
Siku ukizaliwa nitarudia, teana kwa sauti na utanisikia, sitaki kukuonya kuhusu dunia, sababu dunua ipo na utashuhudia,najua husikii ninayokwambia ila ukizaliwa nitarudia,
ukizaliwaaaaaaaaaaa x3
Najua husikii ninayokwambia
Ila ukizaliwa nitarudia
Naomba uyatii ninatokwambia
Maana yadunia yanavutia
Kwahiyo ukizaliwa mama, ukizaliwa mama