Kale nilitembea Lyrics
- Genre:Gospel
- Year of Release:2022
Lyrics
Kale nilitembea - Beatrice Mwaipaja
...
Kale nilitembea, nikilewa dhambi
Nilikosa msaada, kuniponya mateso,
Hata nilipofika, Mahali pa Msalaba,
Palinifaa sana, Sitasahau kamwe,
Hicho ndicho chanzo,
Cha kufurahi kwangu
Hapo ndipo mzigo, Uliponituliwa.
Usifiwe Msalaba!
Lisifiwe kaburi!
Linalozidi yote,
Asifiwe Mwokozi!
Panapo msalaba, Kinatolewa cheti,
Cha kuingia Mbinguni, Kisicho cha kanisa
Yule Bwana mjinga, Likwenda bila cheri,
Kitumai kwingia, Kama walio nacho,
Lipofika langoni, Akaulizwa cheti,
Cha kumwonyesha Bwana,
Akakutwa hanacho.
Usifiwe Msalaba!
Lisifiwe kaburi!
Linalozidi yote,
Asifiwe Mwokozi!
Lituhuzunishalo, Ni ninyi msio nacho,
Kuwa kama mjinga, Kwa siku ya arusi!
Ubavuni mwa Yesu, Mlitokea damu,
Chemchemi ya uzima, Itakasayo roho,
Jitahidi wingie, Damuni mwa Mwokozi,
Utafutiwa dhambi, Toka rohoni mwako.
Usifiwe Msalaba!
Lisifiwe kaburi!
Linalozidi yote,
Asifiwe Mwokozi!