![Siwezi](https://source.boomplaymusic.com/group2/M01/20/C3/rBEeM1uOicCAdGZ2AAEn6A_dWCE628.jpg)
Siwezi Lyrics
- Genre:Bongo Flava
- Year of Release:2018
Lyrics
Siwezi - Beka Flavour
...
Mh, Aaah, Hee he heee....
Kila siku unaniulizaga moja swali,
Hivi lini nitakujaga kuwa vizuri,
Maana kila siku Ahadi, halaf hazitimii,
Sikosi kukupandisha kweny bajaji,
Wakati level zako we ni Lamborghini,
Nakushushaga hadhi,
na uzuri wako huendani..
Kaa ukijua, mgawa ridhiki si mimi ni mola,
Huenda kesho atanipatia,
japo kidogo kunigawia
Ninavyojua mwamvuli hutumikaga wakati wa mvua
Ikinyesha atafunikia pendo letu lisije kuloa,
Amini mama, kukupoteza siwezi,
Ah, na sitoulizia, wengine waipande ngazi
Aah, Amini mama, kukupoteza siwezi,
Ah, na sitoulizia wengine waipande ngazi..
Verse: 2
Subira rafiki yake matumaini,
Ukichanganya na Sala,
Si vyema ujilaumu kuwa na mimi,
Eti Sababu fukara,
Na tena we ndio nyongo Kalia ini,
Usinibwage kabwela,
Penzi langu limeota mizizi chini,
Kumbuka haiwez tena..
Kaa ukijua mgawa ridhiki si mimi ni mola,
Huenda kesho atanipatia,
Japo kidogo kunigawia,
Nachojua mwamvuli hutumikaga wakati wa mvua,
Ikinyesha atafunikia pendo letu lisije kuloa,
Amini mama kukupoteza siwezi, Aaah,
Na sitoulizia wengine waipande ngazi..Aah
Amini mama kukupoteza siwezi, Aaah,
Na sitoulizia wengine waipande ngazi.. Aah
Outro:
Ipo wazi, kipato changu kwako hakikidhi mahitaji,
Na mi nipo radhi, nidundulize kwako nilete mahitaji,
Ipo siku moja nitakuvisha shela,
we na mimi tuuage ukapela,
nikupeleke kwa mkubwa fella,
Ipo siku moja nitakuvisha shela,
we na mimi tuuage ukapela,
nikupeleke nyumbani ifakara..