![Kama Siwezi](https://source.boomplaymusic.com/group10/M00/09/12/5cdcc9671dcb4a15915e56923a55c6ec.jpg)
Kama Siwezi Lyrics
- Genre:Bongo Flava
- Year of Release:2021
Lyrics
Kama Siwezi - Beka Flavour
...
Uuuuuuuuuuuuuuh uuuh
(Mafya)
Mmmh licha ya mapenzi yote kumkabidhi mshahara ni machozi
Mapenzi we yatezame kwa DVD moyo wangu kaupiga shoti
Biashara ya mapenzi mingi mitihani mimi nimeingia loss
Nilipopenda hata sikudhani ningepigwa kidochi
Wanatendwa kina Bill Gate, Shah Rukh Khan sembuse mimi ni nani
Nimekubali najipa imani kuwa yangu ridhiki
Ila kamoyo kana niuma, ila uwoga kanifanyia dhuluma
Mimi nashindwa kuyazoea maumivu yeeh
Bado kamoyo kananiuma, ila uwoga kanifanyia dhuluma
Mimi nashindwa kuyazoea maumivu yeeh
Nitawezana vipi mbona kama siwezi (siwezi)
Penzi lilinikamata siwezi, siwezi
Tururu turu turutu siwzei, siwezi
Penzi lilininogea siwezi, siwezi
Mmh kabomoa daraji angali sijavuka ngambo (ngambo)
Na mimi siwezi ogellllea ata maji ya kisado ( sado)
Kanikomoa kabisa yeye yuko kamili bado (bado)
Yani kama miujiza sijaamini bado (bado)
Moyo kaucharanga chale nyingi amekuwa mganga
Na majini yamempanda mimi si lolote kaniona mshamba
Mimi kwake nilitia nanga vita ya mapenzi yeye kaja na panga
Kanichinja kanicharanga kaniacha niko hoi sijitambui kabisa
Ila kamoyo kana niuma, ila uwoga kanifanyia dhuluma
Mimi nashindwa kuyazoea maumivu yeeh
Bado kamoyo kana niuma, na uwoga kanifanyia dhuluma
Mimi nashindwa kuyazoea maumivu yee eee auuh
Nitawezana vipi mbona kama siwezi, siwezi
Penzi lilinikamata siwezi, siwezi
Tururu turu turutu siwezi, siwezi
Penzi lilininogea siwezi, siwezi
Mbona kama siwezi, siwezi
Siwezi, siwezi
(Mafya)