![Nyota Ya Mashariki](https://source.boomplaymusic.com/group1/M01/7A/9A/rBEeMVsw8hqAFGhBAADv4KIMzGk883.jpg)
Nyota Ya Mashariki Lyrics
- Genre:Afrobeats
- Year of Release:2016
Lyrics
Nyota Ya Mashariki - KMK MAKUBURI
...
Kakukirimia, uwe ulivyo,
Atakutumia impendezavyo
Akikuinua, inuka, hivyo,
Ninakuombea heri vilivyo;
Hakunipa hayo, nikuhitaji,
Kwa niliyo nayo, upate maji,
Na mwisho wa hayo, tuvikwe taji,
Tuingie nayo, wa mbingu mji.
Nimeiona nyota yako mashariki (nyota yako)
Ninajivuna inavyong'ara rafiki (helelelele)
Naandamana kuja unakotamalaki
Kumsujudia Bwana aliyekupa milki (ho ndugu)

Sirudi kwa njia, yake herode,
Anakuvizia, kila upande,
Wivu unamjia, kakunja, konde,
La kukuzuia juu usipande;
Ni kama Kaini, mwua Abeli,
Au Raubeni, wa Israeli,
Waliotamani, kuzika, hali,
Ya wadogo duni, wake Jalali!
Nimeiona nyota yako mashariki (nyota yako)
Ninajivuna inavyong'ara rafiki (helelelele)
Naandamana kuja unakotamalaki
Kumsujudia Bwana aliyekupa milki (ho ndugu)
Nimeiona nyota yako mashariki (nyota yako)
Ninajivuna inavyong'ara rafiki (helelelele)
Naandamana kuja unakotamalaki
Kumsujudia Bwana aliyekupa milki (ho ndugu)
Ninakuombea, usife moyo,
Maana dunia, si rafikiyo,
Wewe fuatia, za Kristu, nyayo,
Aliyekufia, kwa mizigoyo;
Wa ulimwenguni, watakufumba,
Wazuri machoni, moyo mwembamba,
Hawatatamani, uitwe, mwamba,
Ni wivu moyoni, unawasomba!