E.A.S.T (Every Artist Should Teach) ft. Msito & Fedoo Lyrics
- Genre:Hip Hop & Rap
- Year of Release:2023
Lyrics
Huwezi escape reality, na Msito si kidogo/
Na waroga kama sorcery, niko high nyi mko nusery/
Hii kipaji ina ni lisha, ndio maana na heshimika/
Nikifanya na bambika, sense ndio na roga/
Ngoma zenyu zina mangotha, nudity all over, wako uchi bend over/
Hamna teaching mta ni koma, hii level ni mature/
Wana expect ni switch style/
Heri Stamina na Roma/
Me ni mirror kwa society, na sense ni variety/
Kwa game kuna calamity, hii ni masterpiece G/
Wana ni copy me, ma wanna be/
Wana envy me/
I'm making good music, funza wakubwa kwa wadogo/
Maskini na vigogo macho hayaoni kisogo/
Eyoo! East, Every Artist Should Teach/
Mabrother Mafather Mamother Na Makid/
East!, Every Artist Should Teach/
Kwanzia Bara Nchi Mikoa Kata Na Vijiji/
East!/
Ukiacha mademu, kujisifia/
We ni mkali kila ngoma au tungi unavyotupia/
Vipo vingi utaisave jamii ukizungumzia/
Toa funzo wafaidishe watu ulichobarikiwa/
Msanii unaye chora picha au kuigiza/
Unaweza ukawa ticha na ukawaficha ukifundisha/
Embu pata picha,wanao kadhaa wanafanikisha/
Una-solve mabalaa kwa sanaa unayowasilisha/
Ni vipi utaiacha legacy/
Na ikiwa kila track matusi, ni vipi nitakuita legend?/
Mfano Professor Jay alisikilizwa na madingi/
Kina mama, masela watoto shule za msingi/
Au Sugu mapinduzi kwa wasanii nao wapate shilingi/
Kua mhadhiri kama Maalim Nash MC mtaa upate mapindi/
Toa Mapini kama Adam Shule Kongwe SHULE NA SHULE/
Ambao hatukusoma kisa ada tupe shule ya bure/
Eyoo! East, Every Artist Should Teach/
Mabrother Mafather Mamother Na Makid/
East!, Every Artist Should Teach/
Kwanzia Bara Nchi Mikoa Kata Na Vijiji/
East!/