Pumzika ft. Adam Shule Kongwe Lyrics
- Genre:Hip Hop & Rap
- Year of Release:2022
Lyrics
We Ukiskia kupumzika huwa unaelewa nini/
Huenda unavyoelewa wewe sivyo navyoelewa mimi/
Amini kwamba Ila amini usiamini/
Wote tuko sawa tunapozungumzia hili/
Kila mtu hupumzika anavyojua yeye/
Kwa muda na mahali anapokuwa yeye/
Nje au ndani Asubuhi au jioni/
Unatembea, umekaa, umetulia au umembonji/
Utachagua mwenyewe njia ipi ni ipi/
Pumzika uboreshe afya ya akili na mwili/
Punguza stress weka kumbukumbu sawa/
Imarisha kinga ya mwili, mizuka sana/
Vuta pumzi, jipe vi break hata kidogo/
Usiconfuse na uzembe acha kukaza ubongo/
Najua kuwa unaenda resi na mitkasi/
Ila hakikisha daily una rest una relax/
Refresh ka una press F5 kwa keyboard/
Relax jipe break usifanye mambo Kwa mpigo/
Hata ukisoma kwa usongo au michongo dili nyingi/
Kama unapumzisha chombo mwili vipi/
Unapofanya yako huna budi ujipooze/
Punguza mawazo vuta pumzi jinyooshe/
Afya kwanza bwana mentally and physically/
Ka uko sawa uko shega ni ushindi b/
Usingoje mpaka sikukuu na vacay/
Eti ndo upumzike kwenye siku hizo pekee/
Jenga utaratibu, upumzike kila siku/
Mambo ni mengi huwezi finish kila kitu/
Mambo yenyewe sometime yanachanganya yanavuruga/
Sa kwa nini usijitenge na dunia hata kwa muda/
Mfupi, we vuta kiti kaa/
Kisha fanya choice njia Ipi itakufaa/
Fanya tahajudi au practice yoga/
Kama ni kutembea huko outside toka/
Ukirudi, jimwagie maji oga/
Take a shower iwe safi over/
Technique ni nyingi yani zipo kama zote/
Kama unaweza mbona simpo Fanya zote/
Kabla ya kazi,muda wa kazi baada ya kazi/
Tumia hayo ma gap sawasawa kurelax/
Refresh ka una press F5 kwa keyboard/
Relax jipe break usifanye mambo Kwa mpigo/
Hata ukisoma kwa usongo au michongo dili nyingi/
Kama unapumzisha chombo mwili vipi/
Unapofanya yako huna budi ujipooze/
Punguza mawazo vuta pumzi jinyooshe/
Afya kwanza bwana mentally and physically/
Ka uko sawa uko shega ni ushindi b/
Kama Hauko fresh, umestuck, uko tired/
Ukilala una reset, recover, recharge/
Hata usipolala bado sio swala si unanielewa/
Inhale exhale jinyoshe pigwa na hewa/
Ka ulikuwa hupumziki you better start now/ usijiload kazi nyingi mwisho u shut down/
Uuuuh afya kwanza bwana mentally and physically/
Ka uko sawa uko shega ni ushindi b/
Hebu skiza huu mziki vizuri/
Hizo hasira huenda hupumziki vizuri/
Maudhi na kero vitu havishiki vizuri/
Sometime hujigijigi vizuri/
Relaxation sets mood ya kazi na other desires/
Ifanye ka sanaa ifanye kama ni science/
Jitahidi sana na Ufanyage juu chin/
Ongeza kupumzika kwenye daily routine/
Kupumzikaa ni jambo la mbolea jo/
Na sio mpango ukachorea jo/
We do biz piga shugli bana/
Ila hakikisha unapumzikanga/...
Yeah! Yaliyosemwa yafanyike/
Nimeshachana ngoja nikapumzike/
.... Na hii ni Shule na Shule Micshariki yeah yeah!!!