Mikopo ft. Adam Shule Kongwe Lyrics
- Genre:Hip Hop & Rap
- Year of Release:2022
Lyrics
Sina tafiti yoyote ila nabonga kwa ujasiri/
Kwamba wote mnajua kuwa kukopa ni nini/
Na ili mada iwe tamu uskute wote mnadaiwa hapa/
Mnabisha? Mbona wote hamuitikii sasa/
Iza, hiyo ni commercial break/
Haya wote turudini katika mada yetu hii/
Kwanza jiulize kwa nini unakopa/
Jishauri au omba ushauri kabla ya kutoka/
Jua utafanya nini kisha ukakope/
Sio ukope ndo utajua kichwa matope/
Na tafuta mikopo yenye riba nafuu/
Watu wengi wameumizwa kwenye riba za juu/
Kopa kiasi unachoweza kurudisha/
Acha tamaa sifuri unazoongeza utazilipa/
Na Hela nyingi usikope kuanzisha biashara/
Mkopo ni wa kuimarisha biashara/
Hiyo hela inabidi izunguke ili izae/
Ili deni lipunguzwe hawajakupa Ili ikae/
Na achana na biashara za kupata majaliwa/
Kuwa fasta na ambazo ukizifanya uhakika/
Kuwa makini sana na dhamana/
Usije poteza vitu vya thamani na vya maana/
Kama mali sana sana/
Nini samani, nyumba zinauzwa mchana mchana/
Mikopo ina ubaridi na joto la maana/
Mikopo ina faida na mikopo ina hasara/
Yani ina pande mbili ka sarafu/
Kwa hiyo cheza kwa akili acha rafu/
Ukiliwazwa na matunda ya ukimaliza kulipa/
Waza na za hatua za ukishindwa kulipa/
Kuwa makini na mikopo tuliza akili kwa mikopo/
Kuna utajiri kwa mikopo na umaskini kwa mikopo/
Mara tu unapopewa usizuzuke na pesa/
Sababu za kuombea uzikumbuke mapema/
Mzee wangu acha kukopa ukaponde raha/
Kula nyama choma kugonga mapombe bar/
Na mamdogo unauchubua ka huskii/
Usitegemee mkopo kununua waksi/
Au Kupika kupakua mahanjumati/
Kulumbua ili kuwaumiza pua majirani/
Mikopo yenye faida ni ile inayokimbiza lengo/
Yenye tija ile Inayotimiza lengo/
Ile ambayo ikiisha inakuacha umesogea/
Piga mahesabu uone umepata umepotea/
Kila ukitaka kulala kumbuka unadaiwa/
Hii itafanya uwahi kuamka na hasira/
Kudamka na dhamira ya kutafuta ngawira/
Kungachamka ili mifuko iweze umuka ka ina hamira/
Ka malipo ni ya awamu aisee acha mchezo/
Zingatia sana tarehe ya marejesho/
Ili kuepuka fine au adhabu/
Usilale au ukae uandae na sababu/
Kumbuka fine kama utumbo itakujazia nzi/
Utachelewa kumaliza itakupunguzia speed/
Ukijiskia uvivu kukomaa hata kidogo/
Rudi Kasome tena masharti ya mkopo/
Mikopo ina ubaridi na joto la maana/
Mikopo ina faida na mikopo ina hasara/
Yani ina pande mbili ka sarafu/
Kwa hiyo cheza kwa akili acha rafu/
Ukiliwazwa na matunda ya ukimaliza kulipa/
Waza na za hatua za ukishindwa kulipa/
Kuwa makini na mikopo tuliza akili kwa mikopo/
Kuna utajiri kwa mikopo na umaskini kwa mikopo/
Yeah, Wazoefu wanakwambia siku zote/
Kama hakuna ulazima usikope/
Maana Kukopa harusi ila kulipa matanga/
Kukopa ni nuksi acha kuita majanga/
Unaambiwa usikope kisa flani amekopa/
Au umetamanishwa na tangazo ukanyooka/
Ule ulimi mtamu wa afisa mikopo/
Usikuchanganye maana akibadilika ni nyoko/
Hujaskia mtu amekimbizwa madeni/
Anaishi kwa mashaka anajificha na hahemi/
Heh!! Akiskia hodi tu presha/
Hata usingizi hauoni anakesha/
Unacheza. Watu wanafilisiwa kutwa kucha/
Wapo waliokimbia familia wakazisusa/
Wapo waliopata magonjwa mpaka sasa hawajapona/
Waliobahatika kurudi wengi wao wamekoma/
Mikopo inatesa saa zingine inaua/
Sio maskini tu hata matajiri wanajuta/
Ila ukituliza kichwa na ukaenda na muda/
Ukajifunga kabisa mbona utayapenda matunda/
Jifunze kwa wale walioinuka kwa mikopo/
Jifunze zaidi kwa waliokutwa na mikopo/
Ningekwambia kuhusu Serikali na mikopo/
Ila kuweka roho rehani ndio sitakagi hiyo mikopo/.