Kuza ft. Adam Shule Kongwe Lyrics
- Genre:Hip Hop & Rap
- Year of Release:2022
Lyrics
Haijalishi kwamba uko level gani ya kimasomo
O level, advance au chuo flani unasoma
Unajengwa kuajiriwa uje upate kazi nzuri
Ni vizuri tena soma kwa usongo na ukaze msuli
Kila hatua piga mabanda na high marks
Pepa zijae pass kuwa mjanja like that
Kimbiza ndoto zako za nataka kuwa nani
Ila chkua mbili tatu kabla ya kuja mtaani
Nakupa moyo kuwa mitkasi itatiki
Ila siwezi kukudanganya kuhusu hali ya nchi
Kwenye sekta binafsi na serikali ni mtiti
Michongo haionekaniki hiyo ndo hali halisi
That's why niko hapa kuna kitu tushee
Muhimu sana na inabidi nikugee
Hicho kitu kinaitwa plan b
Huenda wengi wanakijua ila hawakuambii
Naamini mbali na shule una talanta nyingini
Uwezo wa kufanya jambo swadakta ki umahiri
Kiumahiri hata kama sio talanta
Ila unaweza kujifunza na uka masta
Na ukaliboresha ukajikuta umelijua
Na ukajua kwamba litakuinua ukiamua
Anza kudeal nalo usingoje shule iishe
Ongeza maarifa jifunze jiivishe
Mwambie mzazi kipi unaweza fanya
Sema mapema kitu unachopenda acha kukwama
Niko sure, hawezi kataa kukusapoti
Kama lengo ni kuishi poa na kushika noti
Ikitokea huna mashavu ya ajira
Huwezi kuwa disappointed ghadhabu na hasira
Nna hakika, huwezi kupoteza mitaji
Zaidi ni kuwekeza kuendeleza kipaji
Na kuendeleza si kazi, kazi kuanza moja
Kujitafuta mpaka ujipate huwa ni noma
Na uchumi wa nyumbani wengi hatuna pesa nyingi
Unaweza kumtesa dingi mikopo na pressure nyingi
Ndugu! Sasa yote ya nini
Wakati namna ipo ukijenga msingi
Badala ya kungoja ajira wakati muda unakwenda
Au kufanya kazi ambayo hata hujaipenda
Au kuwa chini ya mtu na kumtumikia
Utajiajiri na mwisho wa siku utafanikiwa
Start slow start small utagrow fast and bigger
You just trust the process huo wakati utafika
Tafakari chukua hatua ka wasemavyo haki elimu
Hii vita utaishinda ukikamata hizi mbinu