It's a wRap! ft. Adam Shule Kongwe Lyrics
- Genre:Hip Hop & Rap
- Year of Release:2022
Lyrics
Tulianza na shujaa tukiongelea lupus/
Tukawafunza kwa kina tukawapea full track/
Ikafuata watoto na michezo/
I hope wenye watoto walifuata maelekezo/
Na asili halisi ilihusu tiba mbadala/
Uzima nje ya hospitali bila mlima wa dawa/
kisha zoeza matizi one two/
Tukawaamsha kupasha kuwa fiti huwa ni cool/
Ndipo tukaenda kwenye elimu siha/
Swala la pedi kwa moja nyingi tukagusia/
Na kwenye unao tuliungumzia muda/
Kwa mifano kibao kuuangalia kwa ukubwa/
Ile siku nzima anayopewa mwenye pumzi/
Utachagua ku use it au ku make excuses/
Sio poa!!!! Nikazama kwenye sanaa/
Tukajua isingekuwepo duniani ingekuwa balaa/
Ikaja baraka iliwagusa wengi/
Maana ulimwengu wa vitu umepofusha wengi/
Ndio maana tunapaswa kujifunza iqra/
Soma, learn, jua elimika/
Niliandika na barua kwa mzazi au mlezi/
Kumkumbusha nafasi yake kwa ukuaji na malezi/
Kwa ujumbe, shule na shule ni funga kazi/
Rapper gani angeongelea umuhimu wa kunywa maji/
Sema shule na shule, Micshariki/
Shule na shule, Micshariki/
Shule na shule, Micshariki/
Shule na shule, Micshariki/
Picha kibao watu wanamtumia adamu/
Wanaposema naenda kuchangia damu/
Mada kubwa iliyokuja ikaja shusha mkono/
Kukemea unyanyasaji wa wanawake kila kona/
Vijana wadogo tuliwafunza kujiamini/
Kukuza vipaji na ujuzi ili kuja kujiajiri/
Na kwenye mistari ya humu/
Ulioongelewa sana ni ule wa sukari ya zuchu/
Wa siku ile kwenye kikao cha night/
Tulipowekana sawa sisi kama wapangaji/
Baada ya hapo ilifuata pumzika/
Nikijiita dr kongwe hampaswi kuuliza/
Msidanganywe na mitandao/
Itumieni kuwa chanya mkikwama tutawasahau/
Mi sikuupuza kuhusu afya akili/
Kipindi cha funguka hakikuacha hili/
Usalama na afya kazini/
Nilivaa vifaa kinga nikamwaga madini/
Kwenye zam kwa zam nako sikukaa pembeni/
Na wastaarabu wenzangu wasioharibu foleni/
Huku nikisanua wengi kuhusu mikopo/
Niliowasaidia nipeni ruzuku kidogo/
Kwenye maisha ulinzi lazima/
Ndo maana nikashusha stanza za umuhimu wa bima/
Tukamaliza na michango kuchangisha kistaarab/
Na leo tunafunga Its A wRap/
Sema shule na shule, Micshariki/
Shule na shule, Micshariki/
Shule na shule, Micshariki/
Shule na shule, Micshariki/
Shukran kwa wote mliofanikisha/
Mlionipa mada nyie pia mlitisha/
Kwa msaada wa mtandao na kuwasumbua ninyi/
Mmemjenga shule yao anko amejua vingi/
Nimekuwa busy nakesha nikichora/
Asante micshariki na kefa mkombola/
Asante punisher, fighter na rama/
Miracle,, unknown na y wa kahama/
Waunda macover lazma nipawaishe/
Walianza watu makini akafuata nikvision/
Ma visitor wa site na youtube channel/
Viewers zaidi ya buku tano/
Huh! Wasikilizaji na walengwa/
Naamini kila mstari utawajenga/
Shule na shule toka mwanzo bila doubt/
Na leo tunafunga its a wrap/