Moja Nyingi ft. Adam Shule Kongwe Lyrics
- Genre:Hip Hop & Rap
- Year of Release:2022
Lyrics
Kuhusu wanawake na elimu siha/
Swala la hedhi huwezi kuacha kuligusia/
Na maswala kama haya kwenye hii dunia tulipo/
Huwezi kusema kwamba kuyazungumzia ni mwiko/
Yeah, yapaswa kujiuliza/
Ni kipi bora zaidi ya afya na uzima/
Iwe mashuleni iwe sehemu za kazi/
Wanawake hupata sana changamoto za usafi/
Kwenye midogo na vijiji/
Huko ndiko, kuna changamoto mara mbili/
Na hupelekea kushindwa kufanya kikamilifu/
Kazi na masomo ushiriki unakuwa hafifu/
Hivyo pedi ni hitaji la msingi/
Kila mmoja anapaswa kujitahidi/
Naamini kivyovyote hatuwezi kukwama/
Kumsaidia mlengwa kwenye hedhi salama/
Na malengo mnayoweka/
Msisahau hoja ya upendo peneza/
Mkitoa elimu bure mzingatie hii/
Kwenye kila shule pedi zigawiwe free/
Sababu hedhi sio kila siku/
Hedhi ni siku chache kwa mwezi so sio issue/
Ya kuifanya serikali ishindwe kugawa bure/
Na kupelekea wasichana washindwe kukaa shule/
Ukifanya hesabu ya haraka/
Utapata ni vipindi mia nne kwa mwaka/
Ambavyo watavikosa sababu ya shida hiyo/
Na mahudhurio kupungua ni tatizo/
Itadumaza ustawi wa elimu ya mwanamke/
Serikali yangu inabidi mchangamke/
Najua kuwa mnajua ila nitarudia/
Ukimwelimisha yeye umeelimisha dunia/
Hata wale wanaobaki na kukaa majumbani/
Bado hali zao sio salama sio shwari/
Vitu wanavyotumia kujisitiri sio uhakika/
Kuna hatari ya kupata maradhi na kudhurika/
Why wakose raha na kukumbatia unyonge/
Ee, wakati hedhi sio ugonjwa/
Mimi naona kama miyeyusho/
Yani binti asiwe huru kisa uhaba wa taulo/
Na haishindikani pedi kuwepo kila kona/
Haswa kule ndani ndani zipelekwe za kutosha/
Wanaozua wapunguziwe kodi iwe poa/
Bei ishuke na bidhaa ziwe zenye bora/
Salute kwa dada Flaviana/
Taasisi yako inafanya makubwa safi sana/
Sisi kwa wingi wetu hatushindwi kuchangishana/
Na kufanya pedi ziwe rahisi kupatikana/