Naenda ft. Adam Shule Kongwe Lyrics
- Genre:Hip Hop & Rap
- Year of Release:2022
Lyrics
Hapo zamani nilikuwa sifaham/
Sikuelewa kabisa mambo ya utoaji dam/
Ukichanganya na story zilizokuwepo mitaa/
Ndo kabisaa, ungeniambia ningeleta balaa/
Ebwana ee, kumbe watu wanakufa/
Afu si tunadanganyana eti damu itauzwa/
Haya mambo ni mazito man/
Usichkulie sio sio sio simple man/
Cheki idadi kubwa ya wahanga wa ajali/
Bado kuna wagonjwa wa upasuaji/
Cheki kina mama wajawazito and/
Wale watoto wenye sickle cell/
Wanahitaji sana damu hata kupita maelezo/
Nasisitiza hata kupita maelezo/
Kila siku, wanahitaji damu ka chakula/
Tena nyingi kwa hiyo inabidi kuwe damu ya dharura/
Sihitaji wa kunishawishi au kukomaa sana/
Najua damu haizalishwi maabara/
Zaidi ya kwa binadamu hakuna pa kuipatia/
Hakuna namna nyingine zaidi ya kuchangia/
Naenda sasa naenda now/
Wenye utayari kama mimi wote naenda nao/
Kuchangia ni hiari naenda kwa hiari yangu/
Naenda kuokoa maisha raia wenzangu/
Nenda sasa nenda now/
Wenye utayari kama wewe wote naenda nao/
Kuchangia ni hiari nenda kwa hiari yako/
Nenda kaokoe maisha raia wenzako/
Naenda leo mi siwezi kukaa tu/
Mwanaume anachangia kila miezi mitatu/
Kina dada kina mama ni miezi minne/
Mtu mwenye vigezo iweje ushindwe/
Hakikisha kwamba umri unaruhusu/
Miaka 18 mpaka 60 au pungufu/
Uzito ni kuanzia kilo 50 kwenda juu/
A donor must have at least 50kgs/
Usiwe mgonjwa wa presha na kisukari/
Usiwe katika tiba hata iwe tiba gani/
Usiwe na magonjwa ya ngozi au kifafa/
Naamini umenielewa of course umenipata/
Kwa mwanamke kuna kitu cha kuongeza/
Usiwe mjamzito au unayenyonyesha/
Kigezo kingine kwa kila mchangiaji/
Asiwe na mwenendo sababishi wa maradhi/
Maradhi hayo ni yale ya kuambukiza/
Mwenendo ni ngono zembe madawa na ulevi pia/
Kuna vigezo vingine nimeviruka?/
Sio kesi watataja nikienda nitavikuta/
Naenda sasa naenda now/
Wenye utayari kama mimi wote naenda nao/
Kuchangia ni hiari naenda kwa hiari yangu/
Naenda kuokoa maisha raia wenzangu/
Nenda sasa nenda now/
Wenye utayari kama wewe wote naenda nao/
Kuchangia ni hiari nenda kwa hiari yako/
Nenda kaokoe maisha raia wenzako/
Ka ni salama kutoa niseme ntaogopa nini/
Watapima vvu kaswende na homa ya ini/
Majibu yanakuwa siri ka uendapo kwa daktari/
Na watacheck mtoaji damu yake kundi gani/
Na kiwango! Lazima kujua ni kitu poa/
Watafuata utaratibu hawafikii kutoa/
Ka umeguswa na unataka ukatoe we shika njia/
Hakuna madhara yoyooote ukichangia/
Ila kwenye faida hapo zipo kedekede/
Yeah, tulia nikuelekeze/
Hupunguza athari ya saratani au cancer/
Hatari ya magonjwa ya moyo na mishipa husepa/
Ukitoa mfululizo kipindi cha miaka sita/
Na kuburn calories pia inakuwa uhakika
Kwa kuwa kila muda ukifika unapimwa/
Unaweza kugundua una ugonjwa na ukaanza tiba mapema/
Yote tisa, kumi ndio mwisho kitu ambacho/
Ni kuokoa maisha ya raia wenzako/
Na hujafa hujaumbika bora kuwa mchangiaji/
Huenda kesho ukawa ni wewe au nduguyo anahitaji/
Na kusema damu itauzwa ni uongo wazo chafu/
Hakuna kitu cha thamani kama damu/
Hii damu haiuzwi inagawiwa bure/
Na siku ukihitaji utapatiwa bure/
Na kama ni mchangiaji utapewa kipaumbele/
Pia kumbuka ni hiari uamuzi unao wewe/
Moja/
Na usiseme sijui dini haijaidhinisha/
Kuchangia damu ni zawadi ya maisha/
Na kabla hujasema na mi ni mtu/
Jiulize kama unathamini utu/
Toa damu anza leo acha kusema bado kwanza/
Usingoje matukio au yakitokea mabonanza/
Mi naenda sasa naenda now/
Na wote walio tayari waje niende nao/
Hii ni shule na shule Micshariki