Shusha Mkono ft. Adam Shule Kongwe Lyrics
- Genre:Hip Hop & Rap
- Year of Release:2022
Lyrics
Shida kidogo tu murder kill kill/
Kweli magonjwa ya akili ni real/
Unachinjaje mtu kisa kakukataa/
Sababu nyingine unashindwa hata kushangaa/
Aaa na hizi ndoa za kufosi/
Tunafosi sana mwisho tunazoa na mikosi/
Mtu ukimuoa bila yeye kupenda/
Ana asilimia kubwa kuwa na wenge la kwenda/
Kingine ni tamaa ndogo ndogo/
Wife unaye bado unakaa kwa dogo dogo/
Bronzo ishirikishe akili/
Kama vipi muhalalishe mfanye mke wa pili/
Mara wivu wa kimapenzi unakuteka unaongoka/
Hujui ka unaumwa unateswa na sonona/
Mwisho mapanga na tindikali/
Unamuua mwanamama kinyama hata hujali/
Huyu nimesomesha yule nimelea mimba/
Huyu nimempa mtaji yule nimejengea nyumba/
Tuliza ndonga bro utaua wangapi/
Shusha mkono mambo hayo sasa basi/
Shusha mkono!! Acha unyanyasaji!!
Shusha mkono!! Huo sio ushababi!!!
Shusha mkono!! Badilisha itikadi!!!
Shusha mkono!! Zuia mauaji!!
Kabla hatujauliza is it love or shillings/
Tukubaliane kwanza kwamba no more killings/
Kabla hatujatafuta chanzo ni bwana au bibi/
Tushushe mikono kwanza au vipi/
East africa, mbona unyanyasaji unakithiri/
Kutwa visa ka utitiri na mauaji ya kikatili/
Hii miaka miwili wanawake wanazidi kaa/
Yani kenya pekee ni zaidi ya sitini na/
Bado bongo uganda na nchi zilizobaki/
Story ni nyingi kuliko walizo publish/
Waliozeshwa mapema haijatosha/
Wengine walikeketwa haijatosha/
Walikuwa mpaka chombo cha starehe na haijatosha/
Wakanajisiwa kisa fedha haijatosha/
Saivi imekuwaga kifo ndo suluhu/
People are so evil unyama ndo umekubuhu/
Duuh! Na hii mifumo dume/
Ndo inafanya tuone kwamba wanawake wakikosea wana haki ya kuchezea wanastahili hata wakufe/
Tuiangalie kama sio ivunjwe vunjwe/
Tucheki njia nyingine ila mikono ndio ishushwe/
Licha ya kuwepo mashirika na wadau mbalimbali/
Most of the time haki za binadamu hazifuatwi/
Sheria zimetungwa na hazina maana/
Msaada hautoki hata kimahakama/
Utaskia tunafanyia upepelezi/
Na hawachukulii serious kufuatilia kesi/
Ndio maana wahanga hata polisi hawaendi/
Maana hawazingatiwi wanakalishwa sana benchi/
Wakikumbuka kero na kuombwa rushwa/
Wengi wanakataa tamaa na kuanza kungoja kufa/
Oya wakubwa ambao bado hamjashtuka/
Kisa bado hamjakumbwa au bado hamjaguswa/
Shit serious and not funny remember/
A next victim might be one of your family members/
Na watu wengine ambao wapuuzi sana/
Ni wenye dough, viongozi wanao misuse power/
Upuzi sana hizi groups bana/
Zapaswa kuwajibishwa kabla ya issues za karma/
Msiposhusha mikono mjue tu iko day/
Mtashikwa na mtahukumiwa, muwe condemned/..