![Unao ft. Adam Shule Kongwe](https://source.boomplaymusic.com/group10/M00/09/16/0762a7ab3f8a4da09babc66d32b0e8ef_464_464.jpg)
Unao ft. Adam Shule Kongwe Lyrics
- Genre:Hip Hop & Rap
- Year of Release:2022
Lyrics
Kuhusu wanawake na elimu siha
Swala la hedhi huwezi kuacha kuligusia
Na maswala kama haya kwenye hii dunia tulipo
Huwezi kusema kwamba kuyazungumzia ni mwiko
Yeah, yapaswa kujiuliza
Ni kipi bora zaidi ya afya na uzima
Iwe mashuleni iwe sehemu za kazi
Wanawake hupata sana changamoto za usafi
Kwenye midogo na vijiji
Huko ndiko, kuna changamoto mara mbili
Na hupelekea kushindwa kufanya kikamilifu
Kazi na masomo ushiriki unakuwa hafifu
Hivyo pedi ni hitaji la msingi
Kila mmoja anapaswa kujitahidi
Naamini kivyovyote hatuwezi kukwama
Kumsaidia mlengwa kwenye hedhi salama
Na malengo mnayoweka
Msisahau hoja ya upendo peneza
Mkitoa elimu bure mzingatie hii
Kwenye kila shule pedi zigawiwe free
Sababu hedhi sio kila siku
Hedhi ni siku chache kwa mwezi so sio issue
Ya kuifanya serikali ishindwe kugawa bure
Na kupelekea wasichana washindwe kukaa shule
Ukifanya hesabu ya haraka
Utapata ni vipindi mia nne kwa mwaka
Ambavyo watavikosa sababu ya shida hiyo
Na mahudhurio kupungua ni tatizo
Itadumaza ustawi wa elimu ya mwanamke
Serikali yangu inabidi mchangamke
Najua kuwa mnajua ila nitarudia
Ukimwelimisha yeye umeelimisha dunia
Hata wale wanaobaki na kukaa majumbani
Bado hali zao sio salama sio shwari
Vitu wanavyotumia kujisitiri sio uhakika
Kuna hatari ya kupata maradhi na kudhurika
Why wakose raha na kukumbatia unyonge
Ee, wakati hedhi sio ugonjwa
Mimi naona kama miyeyusho
Yani binti asiwe huru kisa uhaba wa taulo
Na haishindikani pedi kuwepo kila kona
Haswa kule ndani ndani zipelekwe za kutosha
Wanaozua wapunguziwe kodi iwe poa
Bei ishuke na bidhaa ziwe zenye bora
Salute kwa dada flaviana
Taasisi yako inafanya makubwa safi sana
Sisi kwa wingi wetu hatushindwi kuchangishana
Na kufanya pedi ziwe rahisi kupatikana