![Usalama Na Afya ft. Adam Shule Kongwe](https://source.boomplaymusic.com/group10/M00/09/16/0762a7ab3f8a4da09babc66d32b0e8ef_464_464.jpg)
Usalama Na Afya ft. Adam Shule Kongwe Lyrics
- Genre:Hip Hop & Rap
- Year of Release:2022
Lyrics
As long as unapewa chako unatembea/
Iwe mshahara au kifuta jasho unapokea/
Na kesho unarudi tena na kazi inaendelea/
Ndo unajikuta unafanya kazi kimazoea/
Cha msingi mkono uende kinywani/
(au sio) na watoto waende uani/
(namna hiyo) , muhimu unaingiza cash flani/na kazi ni halali wala haijalishi kazi gani/
Ndivyo ilivyo vivo hivyo hilo liko wazi man/
Ila jiulize kazi yako ina usalama kiasi gani/
Yaani! Mazingira ya kazi yakoje/
Ni salama au kuna hatari yoyote/
Sio sababu haujawahi kudhurika/
Ndio iwe guarantee kuwa hupaswi kujiuliza/
Majuto ni mjukuu ni vizuri ukabadili/
Usiishie kuridhishwa na kauli ya mwajiri/
Yeah! Kauli ya tajiri au bosi/
Bila wewe kuchunguza mazingira haitoshi/
Hili swala ni la kufanyia kazi kwa pamoja/
Ni lazima kuzuia ajali na magonjwa/
Hakikisha usalama na afya kazini/
Usalama na afya kazini/
Hakikisha usalama na afya kazini/
Usalama na afya kazini
Hakikisha usalama na afya kazini/
Usalama na afya kazini/
Hakikisha usalama na afya kazini/
Usalama na afya kazini
Kwa kuwa bado mapema yani bado alfajiri/
Well.. Ngoja nianze na mwajiri/
Kama sheria peke yake inatosha unatuambia/
Mbona kuna watu wanakufa na kuumia/
Law pekee hazileti usalama kazini/
Ni wajibu kujilinda na kuwalinda wengine/
Toa mafunzo kwa miaka miwili mara moja/
Kila mtumishi ahudhurie bila kukosa/
(ili) aelimishwe anayofaa kutekeleza/
Iwe vifaa au mashine anayofaa kuendesha/
Wape tahadhari toa maelezo na maagizo/
Waingie salama na kutoka hivyo hivyo/
Weka vifaa vya usalama kwa kila mtu/
Maana afya na usalama ni haki ya kila mtu/ukiwa mwajiri ni lazima/
Utoe kifaa cha kinachofaa cha kulinda, ikiwa wafanyakazi wanaachwa wazi kwa mazingira ya kuumiza..
Ppe wanaita/ yeah!
Na ppe inayohitajika inatofautiana kulingana na kazi inayofanyika/
Kusiwe na hatari ya kitu chochote/
Iwe vifaa, wanyama, ama sumu yoyote/
Na pia.. Hakikisha usafi unaostahili/
Toa maji kwa wingi/
Na idadi ya kutosha ya vyoo nayo ya msingi/
Na pia mahali wanapobadili nguo wafanyakazi , na mahali wanakopumzika wafanyakazi nako ni muhimu pawe safi na sahihi/
Na kumbuka, unapowafanyia yote hayo/
Sio ruhusa kuwakata kwenye mishahara yao/
Hakikisha usalama na afya kazini/
Usalama na afya kazini/
Hakikisha usalama na afya kazini/
Usalama na afya kazini
Hakikisha usalama na afya kazini/
Usalama na afya kazini/
Hakikisha usalama na afya kazini/
Usalama na afya kazini
Baada ya vingi vya kumwambia/
Bosi.. Nafunga kipindi na waajiriwa/
Kwanza.. Msipende mambo ya kurahisisha/
Msianze kwanza kazi kabla ya kuhakikisha/
Uzima wa miundo mbinu hadi milango madirisha/
Vyumba vina hewa na mwanga wa kuridhisha/
Kisha vaeni vifaa vya kujilinda/
Hata kama vinachosha ila vitawakinga/
Na msione ka karaha ndogo ndogo/
Mkishatumia msiache vifaa hovyo hovyo/ kama kuna maji yanamwagika yakaushwe/
Kama kuna vumbi linazalishwa lifutwe/
Kumbuka na kuzima unapowasha umeme/
Na kama kuna nyaya zimechubuka useme/
Usisite kuripoti unapoona tatizo/
Usipuuze chochote upewapo angalizo/
(na ni hatari) kufanya kazi kupindukia/
Nchi nyingine hichi ni kinyume na sheria/
Mtu aliyechoka ni rahisi kukosea/
Haya sio maneno yangu ni tafiti zinaongea/
Usiume kisa unataka ufanyakazi bora/
Ofisi haikui kwa vifo na wafanyakazi wagonjwa/
Hadi hapo sina kingine cha kusema/
Nimemaliza zaidi niwatakie kazi njema/