Funguka ft. Adam Shule Kongwe Lyrics
- Genre:Hip Hop & Rap
- Year of Release:2022
Lyrics
Kwenye mitaa hii tunayokaa ama ku settle
Na kupitia maisha ya furaha na mateso
Kuna watu
Tunawafaham hadi kesho
Wanaficha vingi nyuma ya tabasamu na vicheko
Mfano wanandoa hawana noma wanachekeana
Wako poa hata wakitoka na mikono wanashikana
Hakuna tofauti yoyote wanaoneshana
Ila nyuma ni usaliti na sivyo inavyoonekana
Wanavyoishi utahisi hawajaweza kung'amua
Ila ukweli ni kwamba kuna mwenza kashajua
Au mtu anajua ana ugonjwa
Unammaliza taratibu anakufa anajiona
Cha ajabu kanyamaza ana battle kimya kimya
Na anatamani msaada anapaswa kusaidiwa
Kuna mifano lukuki kaka
Watu wanaficha mengi moyo wa mtu kichaka
Kinachosikitisha na kuchosha hadi saizi
Kwa mambo ya kufikirika wanakosa usaidizi
Usikae na kitu funguka
Kunyamaza sio ishu funguka
Bwana hakuna shida funguka
Bibi vunja ukimya funguka
Pengine kwa sababu ya kuogopa kutengwa
Au kwa sababu ya kuogopa kuchekwa
Au hata kwa sababu ya kuogopa kusemwa
Unakuta mtu ana tatizo na anaogopa kusema
"vipi nikisema na nikakosa msaada
Naweza nikajieleza na nikaongeza msala
Tatizo langu linaweza kuwa aibu
Japo nalenga kujenga ila naweza kuharibu
Ukaribu, undugu mahusiano vile vile
Vinaweza kuvunjika watu hawana simile/"
Badala kukata shauri amwambie flani na flani
Anaamua kuchagua aumie ndani kwa ndani
Coz hakuna anayependa kuonekana ni weak na
Hakuna anayependa kuonekana mjinga
Kwa kifupi tumejijengeaga utamaduni
Kuwa hakuna anayependa kuonekana tofauti
Sio mbaya ni sawa kujifariji
Ila ukweli utabaki ukweli hata kama ukijitahidi
Kuficha vile ama kuficha hivi
Ila haiwezi fanya hilo tatizo kupita hivi
Sanasana litazidi kukutafuna
Litazidi kukuvuruga na kuzidi kuwa kubwa
Usikae na kitu funguka
Kunyamaza sio ishu funguka
Bwana hakuna shida funguka
Bibi vunja ukimya funguka
Kama unaminya na kinywa hautafungua/kumbuka mficha maradhi kifo humuumbua
Mimi siwezi nikakuficha skia
Kuna madhara makubwa unapoficha hisia
Na kupelekea vile unavyohofia kwa uchache
Kuja kwa wingi na kukujalia we udate
Asiye sawa hayuko sawa ataonekana
Haijalishi mara ngapi anakazia yuko fine na
Kama wanaokuamini inabidi uwadanganye
Vipi wakijua na wakakosa imani nawe
(Na) stress unayozidisha kuficha na kadhalika
Isipotibika hukaribisha na washirika
Yapo madhara ya kutolala vizuri
Kiafya hapo majanga huja asubuhi
Shinikizo la damu high blood pressure
Magonjwa ya moyo lazima yatakutesa
Sukari nayo haiko mbali ni kugusa
Au) kifo cha mapema haikatai ni kuvuta
Kama kufunguka ndio mwanzo wa kujitibu
Ya nini kuvunga au kujitia uraibu
Au kuwaza kujiua kwa sumu au kamba
Kujining'iniza na kujitesa hadi kudanja
Kabla hujafika huko kifikra hadi kimwili
Acha kujiharakisha subiri
Magumu unayopitia haupitii alone
Humu kwenye dunia hakuna kipya homie
Najua ni ngumu kwa jamii inayokuzunguka
Jipe muda, kisha jiamini kufunguka
Chagua unayemuamini na uliye huru kwake
Iwe mtu, taasisi mtilie maguu mfuate
Mweleze yote na usibakishe kitu
Jiaminishe uaminike usijiwazishe kitu
Unayepigana kuwa sawa kuwa full ni wewe
Kuwa free, ukweli utakuweka huru milele
... Chenye mwanzo kina mwisho yatakwisha
Yamalize urudi utimize mipango maisha
Yalosibu yamesibu simama pambana nayo
Ni ya muda utatulizana utaachana nayo