Simama Imara Lyrics
- Genre:Acoustic
- Year of Release:2022
Lyrics
Niko mbali nawe mpenzi
Wangu wee ninatamani
Niwe nawe daima ooh
Pesa ninakutumia singojei
Mwisho wa mwezi
Mungu ananijalia we
Japo nikikutumia ujumbe mfupi
We majibu yako yanachelewa
Sana oooh
Kila nikikupigia simu
Namba haipatikani
Kila nikikupigia simu
Namba inatumika
Ooooh kuna nini huko
Ooooh kuna nini huko
Mpenzi wangu we usije
Ukahadaiwa
Mpenzi wangu we
Simama imara
Wanaojifanya kukupenda
Sana uwaepuke eh
Nia yao wakutumie halafu
Wakutupe kama bua la muwa
Mpenzi wangu we usije
Ukahadaiwa
Mpenzi wangu we
Simama imara
Mimi nawe tumetoka mbali sana
Nani asiyelijua hilo
Mioyo yetu iache idunde
Kama moyo mmoja oouoh oh
Mpenzi wangu we usije
Ukahadaiwa
Mpenzi wangu we
Simama imara
Pitapita mbele yao huku
Ukiwa umependeza sana
Wacha wahangaike ye yei yeh
Najua watayasema mengi sana
Mimi nitayaziba masikio
Yo yoiyooh
Watasema umelisha limbwata
Ndio maana sishawishiki
Wala sihangaiki yooh
Mpenzi wangu we usije
Ukahadaiwa
Mpenzi wangu we
Simama imara
Wanaojifanya kukupenda
Sana uwaepuke eh
Nia yao wakutumie halafu
Wakutupe kama bua la muwa
Mpenzi wangu we usije
Ukahadaiwa
Mpenzi wangu we
Simama imara
Mimi nawe tumetoka mbali sana
Nani asiyelijua hilo
Mioyo yetu iache idunde
Kama moyo mmoja oouoh oh
Mpenzi wangu we usije
Ukahadaiwa
Mpenzi wangu we
Simama imara