
Nimeachika R&B Lyrics
- Genre:Others
- Year of Release:2024
Lyrics
Nimeachika
Nimetulizana ndani
Kutoka nje najionea taabu
Kila ninayemuona
Kwangu yuko kama adui
Walimwengu mmeniponza
Sijui nitafanyeje
Mimi na yeye turudiane
Eeh turudiane
Mlinilisha story za uongo
Nami bila kuhoji na
Kujihakikishia nilimlaumu
Mpenzi wangu na kumuona
Si wa maana
Nilipuuzia yote aliyonifanyia
Nilimpa kisogo nikamwacha
Anaombeleza
Sasa mnanitakia nini
Ebu mniache kupotea
Ni wakati wa kwenda
Kurudi nina ijua njia
Nimeachika Nimeachika
Mie mie Kwa uzembe wangu
Sina wa kumlaumu
Nimeachika Nimeachika
Mie mie Kwa uzembe wangu
Sina wa kumlaumu
Nilipigiwa simu muda wote
Eti yuko Tandika na fulani
Wengine eti wamemuona
Akipita Pale Kijazi flyover
Pembeni akiwa na mwingine
Akirudi namfokea
Nakasirika wiki nzima
Simsalimii, sili naye chakula
Najuta Najuta mimi
Nimeachika Nimeachika
Mie mie Kwa uzembe wangu
Sina wa kumlaumu
Nimeachika
Nimeachika
Mie mie Kwa uzembe wangu
Sina wa kumlaumu
Sikieni sasa
Acheni kunifuata fuata
Wacheni nijaribu bahati yangu
Niombe msamaha
Nirudiane naye
Mliniponza najuta
Najuta Nimeachika
Nimeachika Mie mie
Kwa uzembe wangu
Sina wa kumlaumu
Nimeachika Nimeachika
Mie mie Kwa uzembe wangu
Sina wa kumlaumu
Turudiane Turudiane
Nisamehe bure Nisamehe