Visingizio Lyrics
- Genre:Others
- Year of Release:2023
Lyrics
Siku uliyo nikemea
Ulidai ulichoka
Tena pia ukaenda kazini
Bila hata ya kuniaga
Usiku uliyo nipiga kofi
Ulidai ulilewa
Tena pia ukaenda kulala
Bila hata ya kuniaga
Jana ilikuwa birthday yangu
Hukuniletea zawadi
Acha kusingizia simu
Kwa kutokukumbusha
Una visingizio gani?
Sikioni hata kimoja
Una visingizio gani
Sikioni hata kimoja
Mpenzi leo siamini
Kwa kunitendea hivyo
Una visingizio gani
Sikioni hata kimoja
Una visingizio gani
Sikioni hata kimoja
Mtendee mwenzio
Vile utakavyo kutendewa
Siku uliyo nunua gari
Bila hata ya kunishauri
Ulilingiza uani
Huku ukinitazama
Nilipigwa na butwaa
Nikajikalia kimya ah
Mapenzi leo ndio wako
Sitavulia tena ah
Mimi nawe tuko sawa ah
Tutendeane haki iih
Una visingizio gani
Sikioni hata kimoja
Una visingizio gani
Sikioni hata kimoja
Sisi wote ni binadamu makosa tumeumbiwa ndio maana kufanya kosa si makosa bali
Kurudia kosa ndio makosa