Sina Makosa Lyrics
- Genre:Acoustic
- Year of Release:2022
Lyrics
Tulikutana kule Zanzibar
Miezi miwili sasa
Imeshakwisha pita
Tuliongea mchana kutwa
Hata usiku pia hatukulala
Aliniambia hajaolewa
Niliamini ya kuwa
Sasa nimeshampata
Wa kuishi naye milele
Tulitalii nchi nzima
Na tukaanza kupanga
Mambo ya ndoa
Sasa mbona ninapigiwa simu
Eti nimeingilia ndoa
Mwenye mke amekwisha
Kutangaza ama zake ama zangu
Jamani
Sina makosa sina makosa
We bwana sina makosa
Sina makosa sina makosa
We bwana sina makosa
Kaa na mkeo ujue mambo
Yanayomfanya atangetange yeye
Sina makosa sina makosa
We bwana sina makosa
Sina makosa sina makosa
We bwana sina makosa
Sina haja na mkeo
Wasio na ndoa
Mbona wako wengi sana
Sina makosa sina makosa
We bwana sina makosa
Sina makosa sina makosa
We bwana sina makosa
Kanipotezea muda
Wangu nitasema nini
Kwa ndugu zangu oooh
Sina makosa sina makosa
We bwana sina makosa
Sina makosa sina makosa
We bwana sina makosa
Tokea leo sina haja na mkeo
Ametufanya tugombane bure
Kaa naye akuambie ukweli
Kama anataka kuishi nawe ooh
Sina makosa sina makosa
We bwana sina makosa
Sina makosa sina makosa
We bwana sina makosa
Tokea leo sina haja na mkeo
Ametufanya tugombane bure
Kaa naye akuambie ukweli
Kama anataka kuishi nawe ooh
Sina makosa sina makosa
Sina makosa