![Pendo La Mungu](https://source.boomplaymusic.com/group10/M00/05/12/dc0541716f20449bb14f7e70f6fd11d3.jpg)
Pendo La Mungu Lyrics
- Genre:Gospel
- Year of Release:2020
Lyrics
Pendo La Mungu - Christina Shusho
...
Naona pendo kubwa mno
Latoka kwa mwokozi wangu
Ni tele kama maji mengi
Yatembeayo baharini
Lanitolea tumaini
ya kwamba nitatiwa nguvu
Na niwe mhodari tena
kwa pendo kubwa la mwokozi
Lanitolea tumaini
ya kwamba nitatiwa nguvu
Na niwe mhodari tena
kwa pendo kubwa la mwokozi
*
Haleluya, ni pendo kubwa
Linalotoka moyo wako
Ee Mungu wangu nakuomba
Nijaze pendo lako tele
Haleluya(Haleluya) ,
ni pendo kubwa (baba)
Linalotoka moyo(moyo wako) wako
Ee Mungu wangu nakuomba (Mungu wangu baba)
Nijaze pendo lako tele
======
======
Na pendo Hilo kubwa mno
Huyaondoa majivuno
Na kunifunza haki Kweli
Uongo wote niuvue
Hunituliza moyo wangu
Huruma nayo hunitia
Na sote tuwe na umoja
Katika pendo la Mwokozi
Hunituliza moyo wangu
Huruma nayo hunitia
Na sote tuwe na umoja
Katika pendo la Mwokozi
*
Hallelujah
Ni pendo kubwa
Linalotoka moyo wako (moyo wako Baba)
Ee Mungu wangu nakuomba
Nijaze pendo lako tele
*
Hallelujah
Ni pendo kubwa
Linalotoka moyo wako
Ee Mungu wangu nakuomba
Nijaze pendo lako tele
=====
=====
Nijazwe pendo hilo kubwa
Linibidiishe siku zote
Rohoni niwe na juhudi
Nimtumikie Bwana Yesu
Hazina Yako nipeleke
Kwa watu waliopotea
Wafahamishwe pendo kubwa
Ulilonalo Mungu wangu
Hazina Yako nipeleke
Kwa watu waliopotea
Wafahamishwe pendo kubwa
Ulilonalo Mungu wangu
*
Hallelujah
Ni pendo kubwa
Linalotoka moyo wako
Ee Mungu wangu nakuomba
Nijaze pendo lako tele
*
Hallelujah
Ni pendo kubwa
Linalotoka moyo wako
Ee Mungu wangu nakuomba
Nijaze pendo lako tele
=====