Akutendee Nini Lyrics
- Genre:Gospel
- Year of Release:2021
Lyrics
Akutendee Nini - Christina Shusho
...
Haleluya!
Yesu ni Bwana!
Na wala Hana mpinzani
Wataka akutendee nini!?
Akutendee nini wee
Wataka akutendee nini!?
Akutendee nini wee
Neno moja nalitaka kwa Bwana
Nalo ni hili,
Nikae nyumbani mwake
Siku zote za Maisha yangu
Ghala lake limejaa
Hakuna aliyepunguza hata robo
Akutendee nini wee
Wengine wataka kuwa Rais wa nchi
Wengine wataka ubunge
Nawe akutendee nini wee!?
Mwingine ombi lake apate shamba
Huyu mume na huyu mke
Wataka akutendee nini wee
Mama huyu ombi lake apate mtoto
Mwingine apate elimu
Wataka akutendee nini wee
Mwambie
Wataka akutendee nini?
(Mwambie)
Akutendee nini wee
(Anasikia mwambie)
Wataka akutendee nini!?
(Atajibu mwambie)
Akutendee nini wee
*
Nina kumbuka mgonjwa birikani
Miaka thelathini na nane
Alikuwa hajiwezi yeye
Yesu akatembelea birika lile
Akamuona mgonjwa yule
Mara akaanza sababu zake
Malaika Akifika anaingia kisimani
Anatibua maji, na mimi nakuwa wa mwisho
Wataka akutendee nini wee
Yesu akasema Neno moja
Jitwike godoro lako na uende
Mara akawa mzima
Hee!
Wataka akutendee nini!?
(Hee mwambie)
Akutendee nini wee
(Mwambie Yesu mwambie)
Wataka akutendee nini!?
(Anasikia mwambie Yesu mwambie)
Akutendee nini(Atajibu mwambie yeye mwambie)
Iyelele mawee!
(Mwambie)
Ee mawee
Iyelele mawee
(ooh mwambie)
Ee mawee
(Usiogope mwambie)
Iyelele mawee
(Ee Mwambie)
Ee mawee
(Acha kulia mwambie)
Iyelele mawee
(Ee Mwambie)
Ee mawee
(Mwambie)
Wataka akutendee nini!?
(Wewe wewe we mwambie)
Akutendee nini wee
(maswali yako yeye Ana majibu)
Wataka akutendee nini
(Vilio vyako yeye atafuta)
Akutendee nini wee
(Mizigo yako yeye atatua)
Wataka akutendee nini
(Ee mwambie we mwambie)
Akutendee nini!?
(Mwambie Yesu mwambie )
Wataka akutendee nini!?
(wewe oh Mwambie)
Akutendee nini wee
(Nami Leo namwambia)