![Machozi](https://source.boomplaymusic.com/group1/M04/AB/79/rBEehlzBg0CAZCyXAADwjAJsZAI063.jpg)
Machozi Lyrics
- Genre:Soul
- Year of Release:2000
Lyrics
Machozi - Lady Jaydee
...
Nimekaa nafikiri
Baadae ninagundua
Kwamba hutorudi tena
Sitokua nawe tena
Lakini najipa moyo
Nione kama ni ndoto
Kwani matone ya machozi
Ni zaidi ya milioni
Machungu tele moyoni
Kweli nimejawa hofu
Sina tofauti na mpofu
Hata njia siioni
Nani wa kunifuta machozi
Moyoni nina majonzi
Sina tofauti na kipofu
Kwani hata
Njia
Siioniii
Aah
Nailazimisha furaha
Ingawa moyoni nna majonzi
Nani wa kunifuta machozi
Umeondoka
Umekwenda mbali
Nailazimisha furaha ingawa moyoni nna majonzi
Nani wa kunifuta machozi
Umeondoka umekwenda mbali
Maumivu tele moyoni
Pale ninapogundua
Kua si ndoto
Bali kweli sitakutazama pembeni
Na kamwe sitasahau
Tabasamu lako tamu
Popote utapokwenda
Kumbuka nilikupenda
Machungu tele moyoni
Wewe kwenda mbali nami
Sina tofauti na mpofu
Hata njia siioni
Nani wa kunifuta machozi moyoni nina majonzi
Sina tofauti na mpofu
Kwani hata
Njia
Siiionii