Siri Yangu Lyrics
- Genre:Soul
- Year of Release:2018
Lyrics
Siri Yangu - Lady Jaydee
...
Nakuambia aa siri yangu
Kwa kuwa wewe ni wangu tena mshikaji siku nyingi,
Nakueleza aa siri yangu inayohusu Maisha yangu inayosumbua moyo wangu.
Tega sikio kwa makini nikuelezee
Hakuna tamu penzi kama la milelee
Muda unaenda mwenzenu mi nagundua
moyoni mwangu katu halitopunguaa
Nimeumizwa mara nyingi nakumbuka
Kuna hatua ilifika mi nikajuta
Lakini sasa na imani yuko wa kumpa
Ninachohitaji ni muda aweze tokea
Siwezi sema kuwa sitopenda tena
Kwani nitakuwa naidhulumu yangu nafsi
Moyoni najua ninalo penzi la milele
Halitokwisha nakwambia labda wa kumpa asizaliwe
Nakuambia aa siri yangu
Kwa kuwa wewe ni wangu tena mshikaji siku nyingi
Nakueleza aa siri yangu inayohusu Maisha yangu inayosumbua moyo wangu
Kuna aliyeniomba nimpatie pumziko
Kwa madai kuwa alichoshwa huko atokako
Niliyempenda nilimwambia nakupenda
Nililia machozi kwa yeyote aliyenitenda
Aliyenichosha nilimwambia waweza kwenda
Kuna aliyenifanya mapenzi yakanitatiza
Niliyemkosea niliona umuhimu wake
Nasisitiza kuwa na penzi la milelee
moyo wanituma wanambia kuwa na subira
Mimi nasema sitoimba tena nalia
Iliyobaki nikusema nimekubali
sitoka tena kulia mimi na mawazo wo wo wo
Nakuambia aa siri yangu
Kwa kuwa wewe ni wangu tena mshikaji siku nyingi
Nakueleza aa siri yangu inayohusu Maisha yangu inayosumbua moyo wangu
Unaweza toa pendo lako kwa furaha
Kumbe moyoni umejijazia karaha
Hutakiwi juta kwani katu hutojua
Unayempenda yeye atakuzingua
Mwisho wa yote ikawa ni matatizo yanayopelekea kuwa na mengi mawazo
Unachotakiwa binti usiusemee moyo kwani
hutojua umpendaye naye akupenda hivyohivyo
Niliwahi kumwimbia mpenzi wangu sema unachotaka ni wimbo uliofatia
lakini pendo hakuna bali ni kutendwa
nimeamua kuwa commando binti machozi
Nakuambia aa siri yangu
Kwa kuwa wewe ni wangu tena mshikaji siku nyingi
Nakueleza aa siri yangu inayohusu Maisha yangu inayosumbua moyo wangu.