Rosella ft. H_Art The Band Lyrics
- Genre:Soul
- Year of Release:2017
Lyrics
Rosella ft. H_Art The Band - Lady Jaydee
...
afraid to tell him how she feels,
she silently whispers to herself ,
afraid ,
holding her breath,maybe
you might hear her
see he doesn't feel the same way
maybe,
h_art the band
Lady Jaydee
Nikaja kupenda na moyo wangu wote
binti huyu aliyefanya nimeuote
usiku na mchana ikawa nikama nimepagawa
sionekani popote
Nikaja kutenda mambo mengine magumu na mazito
ilikuwa mradi niwe naye
Lakini sasa ninapotazama naona kwamba
niliachwa upweke
nilikuwa na wingi wa mahaba
nilikupenda kinyama
kukutenda sikuwaza
kamba nikakaza
Lakini huonekani mpaka sasa
nilikuwa na wingi wa mahaba
nilikupenda kinyama
kukutenda sikuwaza
kamba nikakaza
Lakini huonekani mpaka sasa
Rosella(mi najiuliza)
Rosella(je umebadilika)
Rosella(nashindwa kuamua)
Rosella(mi najiuliza)
Rosella(je umebadilika)
Rosella(nashindwa kuamua)
ni kweli Niliamua kuondoka
nikidhani nitapendwa niendako
oh, hakuna
oh, mi nilidhani nitakuta tofauti yoyote
mpaka sasa sijaona
moyo waniuma, nikikumbuka
mambo mengi Wewe uliyonikosea
najiuliza ni kweli umebadilika
na maumivu mi nayaumia
masikini mi nashindwa amua
oh nashindwa ahaa
najiuliza ni kweli umebadilika
na maumivu mi nayaumia
masikini mi nashindwa amua
oh nashindwa ahaa
Rosella(mi najiuliza)
Rosella(je umebadilika)
Rosella(nashindwa kuamua aah)
Rosella(mi najiuliza)
Rosella(je umebadilika)
Rosella(nashindwa kuamua aah)
yani,imekuwa Siku Mingi sana hatujazungumza
SMS Zangu hurudishi
please call me hunijibu
simu hushiki
najua haiezi Kuwa ni simu umepoteza
juu social media nimeona selfies zako
flani kali
nilikubuyia dashiki
ukweli ni kukumiss nimekumiss tena sana
na najua umenimiss pia
unanilenga tu juu tulikosana
ego Yako iko juu
ulikuwanga dem wa maringo
Lakini siteti
nilikupendanga tu hivyo hivyo
yani tangu unitoke stress iko juu tu sana
Sura imejaza tu mawrinckles
Kila time najipata nimekasirikia tu Vitu simple simple
hata jokes na mapimles nacatch
hao wakishow to madimples
yani Kosa walisema si kosa
kosa ni kurudia kosa
na najua unaniamini ulikosa
but huwezi kubali umekosea
nishakuzoea,ni sawa tu
nimekusamehea
unaact selfish but kuishi bila wewe machozi
misiwezi Yani Kula kwa hoteli si unajua mi ni mwezi
malkia,
smile Tamu,crescent shape ya mwezi
sipendi tukikosana
napenda tukichora Saba kwa saba
loveheart si unajua nakupenda to kwa sana
pamoja tembea Dar twende moshi arusha tunajirusha rusha
spending karibu dolce gabana
mwanaume si unajua ni kujikaza
shopping maspaghetti crop
nine months later baby shower
na pampers
love imeshika rada ladha
firstborn anakaribisha brother
twende nyumbani nikuintroduce kwa Matha
Rosella(mi najiuliza)
Rosella(je umebadilika)
Rosella(nashindwa kuamua)