![Siri Yangu](https://source.boomplaymusic.com/group1/M04/AB/71/rBEehlzBfvCAER0EAADgRuzrqcE18.jpeg)
Siri Yangu Lyrics
- Genre:Soul
- Year of Release:2003
Lyrics
Siri Yangu - Lady Jaydee
...
Nakuambia aah siri yangu
kwa kuwa wewe ni wangu tena mshikaji siku nyingi
nakueleza aah SIRI YANGU inayohusu maisha yangu inayosumbua moyo wangu
tega sikio kwa makini nikueleze
hakuna tamu penzi kama la milele
muda unaenda mwenzenu mi nagundua
moyoni mwangu katu halitopungua
nimeumizwa mara nyingi nakumbuka
kuna hatua ilifika mi nikajuta
lakini sasa na imani yupo wa kumpa
ninachohitaji ni muda aweze tokea
siwezi sema kua sitopenda tena
kwani nitakua naudhulumu yangu sana
moyoni najua ninalo penzi la milele
halitokwisha nakwambia labda wa kumpa asizaliwe.
Nakuambia aah siri yangu
kwa kuwa wewe ni wangu tena mshikaji siku nyingi
nakueleza aah SIRI YANGU inayohusu maisha yangu inayosumbua moyo wangu
kuna aliyeniomba nimpatie PUMZIKO
kwa madai kua alichoshwa huko atokako
Niliyempenda nilimwambia nakupenda
nililia MACHOZI kwa yeyote aliyenitenda
Aliyenichosha nilimwambia waweza kwenda
kuna aliyenifanya mapenzi yakaniTATIZA
Niliyemkosea niliona UMUHIMU WAKE
nasisitiza kuwa kuwa na PENZI LA MILELE
moyo wanituma wanambia kuwa na subira
mimi nasema sitoimba tena NALIA
Iliyobaki ni kusema NIMEKUBALI
sitokaa tena kulia mimi na MAWAZO wow wow woh
Nakuambia aah siri yangu
kwa kuwa wewe ni wangu tena mshikaji siku nyingi
nakueleza aah SIRI YANGU inayohusu maisha yangu inayosumbua moyo wangu
Unaweza toa penzi lako kwa furaha
kumbe moyoni umejijazia karaha
hutakiwi juta kwani katu hutojua
unayempenda yeye atakuzingua
mwisho wa yote ikawa ni matatizo
yanayopelekea kuwa na mengi mawazo
unachotakiwa BINTI USIUSEMEE MOYO
kwani hutojua umpendaye naye akupenda hivyohivyo
niliwahi kumwimbia mpenzi wangu
SEMA UMACHOTAKA ni wimbo uliofatia
lakini pendo hakuna bali ni kutendwa
nineamua kuwa COMANDO BINTI MACHOZI
Nakuambia aah siri yangu
kwa kuwa wewe ni wangu tena mshikaji siku nyingi
nakueleza aah SIRI YANGU inayohusu maisha yangu inayosumbua moyo wangu