![Faraja](https://source.boomplaymusic.com/group1/M01/18/FC/rBEezlthuMmAX-ZsAADycZxm390875.jpg)
Faraja Lyrics
- Genre:Soul
- Year of Release:2018
Lyrics
Faraja - Lady Jaydee
...
Faraja nakutafuta hauonekani?
Mawazo yananitinga moyo unauma faraja oooh!
Uniondoe upwekee, usiniache peke
Dunia imenitupa ndungu wamenitupa oooh!
Pesa hakuna, chakula hakuna
Matatizo makubwa, upweke umenikumba
Pesa hakuna, chakula hakuna
Matatizo makubwa, upweke, upweke, upweke eeh!
Faraja nakuita faraja, uko wapi faraja oooh!
Mawazo yanauwa faraja, nakuhitaji faraja ooh!
Faraja nakuita faraja, ukidhi yangu haja
Dunia inanichanganya, natafuta faraja oooh!
Wapo wengi sana, wakuhitaji faraja
Unikumbuke sana, nami ni wa mmoja
Ukifika kwangu, ukae mwaka mmoja
Tutembee pamoja, nitambe nawe faraja
Lakini ukija leo na uondoke keshoo
Utaniachia mawazo kichwani tele mawazo
Pindi mimi sina pesa, wengine wanatesa
Ninapokua nawaza uwa uwa nakuhitaji faraja oooh!
Faraja nakuita faraja, uko wapi faraja oooh!
Mawazo yanauwa faraja, nakuhitaji faraja ooh!
Faraja nakuita faraja, ukidhi yangu haja
Dunia inanichanganya, natafuta faraja oooh!
Nimezalishwa mwana, baba sijamuona
Nyumba niliyopanga karibu ninafukuzwa
Nimeshauza nyanya, maandazi hata karanga
Faida sikupata, sasa nafa na njaa
Ona barabarani wanavyo omba omba
Nenda kwao faraja, wanakuita faraja
Alau uje sasa ukae nami faraja
Mpaka lini mola maisha haya mabaya oooh!
Faraja nakuita faraja, uko wapi faraja oooh!
Mawazo yanauwa faraja, nakuhitaji faraja ooh!
Faraja nakuita faraja, ukidhi yangu haja
Dunia inanichanganya, natafuta faraja oooh!