Vita Vizuri Lyrics
- Genre:Gospel
- Year of Release:2013
Lyrics
Vita Vizuri - Reuben Kigame
...
Nimevipiga vita vizuri,
Mwendo wangu nimeumaliza
Nayo imani nimeilinda
Natarajia kupewa taji na Bwana.
Nikitazama nyuma sijuti hata
Nimejifunza kusahau yaliyopita
Sasa najisukuma kwa yaliyo mbele
Nikimfuata Yesu mwokozi wangu
Nimevipiga vita vizuri,
Mwendo wangu nimeumaliza
Nayo imani nimeilinda
Natarajia kupewa taji na Bwana
Japo imani yangu imetikiswa
Mimi nimeshikiliwa na Yesu wangu
Hata wakiniacha rafiki zangu
Siri mimi niko na Imanueli
Nimevipiga vita vizuri,
Mwendo wangu nimeumaliza
Nayo imani nimeilinda
Natarajia kupewa taji na Bwana
Nifuateni, nifuatatavyo Yesu
Yeye ni mwanzo na mwisho wa imani yetu
Msishawishike na ulimwengu upitao
Tuvipige vita vizuri
Nimevipiga vita vizuri,
Mwendo wangu nimeumaliza
Nayo imani nimeilinda
Natarajia kupewa taji na Bwana
JOSH MAIMU