![Bwana Mungu Nashangaa](https://source.boomplaymusic.com/group2/M01/6C/3A/rBEeNFqmXT6AZQ-GAADgWxc1Kxw072.jpg)
Bwana Mungu Nashangaa Lyrics
- Genre:Gospel
- Year of Release:2013
Lyrics
Bwana Mungu Nashangaa - Reuben Kigame
...
Bwana Mungu nashangaa kabiisa,
nikifikiri jinsi vilivyo.
Nyota nguruumo vitu vyote pia,
viloumbwa kwa uwezo wako.
(Roho yangu na ikuimbie,
jinsi wewe ulivyo mkuu)×2
Nikitembea kote duniani,
ndege huimba nawasikia.
Milima hupendeza macho sana,
upepo nao nafurahia.
(Roho yangu na ikuimbie,
jinsi wewe ulivyo mkuu)×2.
Tukuza Mungu ni roho yangu,
Sema kabisa jinsi alivyo mkuu.
(ooooh!).
Kristo arudipo kunichukua,
nitabubujikwa na furaha.
tamsujudia mbinguni milele,
natangaza Mungu alivyo mkuu.
(Roho yangu na ikuimbie,
jinsi wewe ulivyo mkuu)×2
(Roho yangu na ikuimbie,
jinsi wewe ulivyo mkuu)×2
jinsi wewe ulivyo mkuu
jinsi wewe ulivyo mkuu.