![Lipo Tumaini ft. Jemimah Thiong'o & Princess Farida](https://source.boomplaymusic.com/group2/M0F/0E/B9/rBEeqF3pFd2ALDfFAACmu-YxjBc708.jpg)
Lipo Tumaini ft. Jemimah Thiong'o & Princess Farida Lyrics
- Genre:Gospel
- Year of Release:2019
Lyrics
Lipo Tumaini ft. Jemimah Thiong'o & Princess Farida - Reuben Kigame
...
Najivika jezi
Wasia kudondoa
Kama Ayubu wa Uzi
Kwa walotiwa doa
Umeshakatwa mizizi
Kisiki lala dongoni
Lipo tumaini
Kwa mti ulokatwa
Maana ukikatwa
Utachipuka tena
2. Wamekupa kisogo
Wa karibu wendani
Kote ni zogozogo
Kunguni kitandani
Hima moyo piga konde
Macho kazia mbinguni
Lipo tumaini
Kwa mti ulokatwa
Maana ukikatwa
Utachipuka tena
3. Jasho ‘lichuruza
Kakubariki Jalali;
Mui ‘kakwaruza
Ikapotea mali.
Umebaki fukara
Wala kwa majalala;
Lipo Tumaini
Kwa mti ulokatwa
Maana ukikatwa
Utachipuka tena
Bridge
Aaaa – sema
Ije gharika – sema
Aaaa – sema
Liwake jua – sema
Aaaa – sema
Ije dhoruba – sema
Aaaa – sema
Tutasimama …………
Aaaa – nyuma
Haturegei – nyuma
Aaaa – nyuma
Tumeshahama – nyuma
Aaaa – mbele
Twaenda mbele – mbele
Aaaa – mbele
Tumelenga …
4. Tuinue tenzi
Wimbo wa rohoni
Kwake mwenye enzi
Waja wa Imani.
Kwa dalili ya maji
Miche itachomoza;
Lipo tumaini
Kwa mti ulokatwa
Maana ukikatwa
Utachipuka tena