![Mbele Naendelea](https://source.boomplaymusic.com/group2/M00/3E/8A/rBEeNFlXw2-AQo-aAADm9hzNlEs918.jpg)
Mbele Naendelea Lyrics
- Genre:Gospel
- Year of Release:2008
Lyrics
Mbele Naendelea - Angela Chibalonza
...
1:Mbele ninaendelea,
Ninazidi kutembea,
Maombi huyasikie,
Ee Bwana Unipandishe.
~Ee bwana uniinue,
Kwa imani nisimame,
Nipande milima yote,
Ee bwana unipandishe.
2:Sinatamani nikae,
Mahali pa shaka kamwe,
Hapo wengi wanakaa,
Kuendelea naomba.
3:Nisikae duniani,
Ni mahali pa shetani,
Natazamia mbinguni,
Nitafika kwa imani.
4:Nataka nipandishwe juu,
Zaidi yale mawingu,
Nitaomba nifikishwe,
Ee bwana unipandishe.
•AMEN