Tabibu Lyrics
- Genre:Gospel
- Year of Release:2010
Lyrics
Tabibu - Angela Chibalonza
...
ooooh...
haleeluhya you are the greatest physician Jesus Christ, son of the living God.
Ni tabibu wa karibu ,tabibu wa ajabu
Na neema za daima, ni dawa yake njema
hatufai kuwa hai, wala hatutumai
ila yeye ndiye atupumuzishaye
imbeni malaika, sifa za Yesu Bwana
pekee limetukuka, jina lake Yesu.
dhambi pia na hatia , ametuchukulia
twenendeni na amani,hata kwake mbinguni.
huliona tamu jina, la Yesu Kristo Bwana
yuna sifa mwenye kufa, asishindwe na kufa
imbeni malaika, sifa za Yesu Bwana
pekee limetukuka jina lake Yesu .
(imbeni eeeeh)
kila mume asimame,sifa zake zivume
wanawake na washike, kusifu jina lake
imbeni malaika sifa za Yesu Bwana
pekee limetukuka jina lake Yesu ×2