![Mteteeni Yesu](https://source.boomplaymusic.com/group1/M00/3E/29/rBEeMllTpmGAYu5vAACJXSVMKCE345.jpg)
Mteteeni Yesu Lyrics
- Genre:Gospel
- Year of Release:2007
Lyrics
Mteteeni Yesu - Angela Chibalonza
...
Mteteeni Yesu,
Mlio askari;
Inueni beramu,
Mukae tayari,
Kwenda nae vitani,
Sisi hatuchoki
Hata washindwe pia
Yeye amiliki.
Mteteeni Yesu,
Vita ni vikali;
Leo siku ya Bwana,
Atashinda kweli,
Waume twende naye,
Adui ni wengi,
Lakini kwake Bwana
Tuna nguvu nyingi.
Mteteeni Yesu,
Wenye ushujaa;
Nguvu zenu za mwili
Hazitatufaa;
Silaha ya injili
Vaeni daima,
Kesheni mkiomba,
Sirudini nyuma.
Mteteeni Yesu,
Vita ni vikali,
Wengi wamdharau,
Hawamkubali,
Ila atamiliki
Tusitie shaka,
Kuwa naye vitani
Twashinda hakika.