Kunapokucha Lyrics
- Genre:Gospel
- Year of Release:2014
Lyrics
Kunapokucha - The Saints Ministers
...
1. Kila kunapokucha, maisha yangu ntakukabidhi, kazi zangu naweka kwako, e Bwana wangu unilinde, Fikira zangu uzing'arishe, ziweze kukuhimidi, Nijaze na roho Mtakatifu.
Chorus
Nikiyafungua macho, nione uwepo wako, na masikio yangu yote, Utulivu uwe wimbo, akili nayo iwaze mema, uniongoze siku nzima, nitalisifu jina lako Bwana unipe matumaini.
2. Siku ikiwa na purukushani, magonjwa mengi yakinibana, ajali huku, sikitiko kote unuzingire Baba, jioni nayo Mungu wangu, neema na fadhili zako, nazihitaji usiku kucha nitashukuru.
Nikiyafungua macho, nione uwepo wako, na masikio yangu yote, Utulivu uwe wimbo, akili nayo iwaze mema, uniongoze siku nzima, nitalisifu jina lako Bwana unipe matumaini.
Bridge:
Kwa mahitaji ya Kesho, sina shaka, kwani wewe Mungu U mpaji.