![Jaba Inampelekanga Mbio Sana !!!](https://source.boomplaymusic.com/group10/M00/05/06/d3cd3d6af9384a35afa649b4193d43f8_464_464.jpg)
Jaba Inampelekanga Mbio Sana !!! Lyrics
- Genre:Pop
- Year of Release:2024
Lyrics
Imekua vigumu Kuchagua marafiki wa kutembea nao
Wanadamu wote wamefanana kama vile punda milia hufanana
Wao huwa marafiki wakati wa shibe na furaha
Wakati amabo wanaweza kunufaika kutokana nawe
Wakati una shida ni wachache sana wanaoweza kukuvumilia na kukaa karibu nawe
Wao hubadilika ukashindwa kuwaelewa ikiwa ni wale mliokua marafiki nao
Huwa inakua vigumu kuamini kabisa kwamba ni wao
Imekua vigumu kuwatafautisha rafiki wa kweli na wasio wa kweli
rafiki akiondoka mwingine akiingia wanafanana taratibu muda ukipita
Yafaa mtu amfae mwenzake wakati wa shida awe na pesa asiwe na pesa hali iwe sawa