Nikumbushe Wema Wako Lyrics
- Genre:Afrobeats
- Year of Release:2016
Lyrics
Nikumbushe Wema Wako - Angel Benard
...
Ni rahisi kinywa kujawa na lawama tele
pale mambo yanapoonekana hayaendi
ni ajabu sana labda moyo unahangaika kutafuta majibu
ajabu sana moyo unavyoonesha mashaka
ya kwamba japokuwa mungu anaishi ndani yetu kuna muda nahofu
japokuwa mungu anaketi kati yetu kuna muda nahofu
nakumbuka wana wa israel katika bahari ya shamu japo walikatisha katikati ya bahari kwa ushind kwa nyimbo nyingi waliimba na kumsifu bwana
lakini baada ya kuvuka na kuliona jangwa yalibadilika mambo
manung'uniko yalisimama aaah
na kusahau muujiza alotenda bwana mungu
eeeh mungu nisaidie