Moyo Lyrics
- Genre:Others
- Year of Release:2024
Lyrics
Vyema mapema
Penzi lako kwenye mizani
Ningepima
Nisingezama
Kwa kina
Penzi lako chungu
Ni ngelitema
Labda kwa kunihurumia
Ungenipa adhabu ya kifo
Milele ningetulia
Nisingesema
Maana nimejikondea
Mithili ya fito
We unajinenepea
Kumbe mapenzi talanta
Sio tu kuzichanga karata
Eti mi sijui kusakata goma
Nimepatikana sikupata
Mishipa ya furaha mwilini umeikata
Et mi sijui kusakata goma
Basi baby nihurumie
Naugua moyo moyo
Naugua moyo moooyo
Naugua moyo moyo
Naugua moyo moooyo
Jua la utosi ardhi ya shaba
Nawezaje kutembea
Bila kivuli chako
Utamu wa nanasi
Umeweka maji
Ladha imenipotea
Supu umeiweka tomato
Ningelikua na uwezo
Kukupa pepo nisingejali
Umejaliwa vigezo
Uwe mke wangu wa halali
Kumbe mapenzi talanta
Sio tu kuzichanga karata
Eti mi sijui kusakata goma
Nimepatikana sikupata
Mishipa ya furaha mwilini umeikata
Et mi sijui kusakata goma
Basi baby nihurumie
Naugua moyo moyo
Naugua moyo moooyo
Naugua moyo moyo
Naugua moyo moooyo