Sabrina Lyrics
- Genre:Bongo Flava
- Year of Release:2023
Lyrics
Sabrina - Tunda Man
...
Juhudi nyingi nimezifanya,
Kukutafuta wangu sabrina
Nimeambiwa mkubwa hapotei,
Emu nambie ka umenikimbia
Matatizo ni mipango ya mungu,
Ambayo sisi tumepangiwa
Najua mimi ndio kidume,
Ambaye napaswa sana kulaumiwa
Umeniachia kidonda,
Ambacho siwezi kukitibia
Pombe inaondoa mawazo
Ila me sina uwezo wa bia
Umeniachia kidonda cha moyo,
Na moyo unauma.
(ahh eh..)
Naona humu muda,
Walau ungerudi nyuma.
(ahh eh..)
Mapenzi ni kupendana,
Mapenzi kusaidiana,
Kwenye dhiki, pia na raha.
Sabrina nakupenda sana,
Naomba urudi mama,
Umeniachia jeraha.
Mapenzi ni kupendana,
Mapenzi kusaidiana,
Kwenye dhiki, pia na raha.
Sabrina nakupenda sana,
Naomba urudi mama,
Umeniachia jeraha.