Jaribu Kwa Mtu Lyrics
- Genre:Afrobeats
- Year of Release:2013
Lyrics
Jaribu Kwa Mtu - Martha Mwaipaja
...
Song: JARIBU by Martha Mwaipaja
Instruments
(Jaribu kwa mtu si kwamba ni mtenda dhambii...ila ni kikombe tuu lazima akinywe
Jaribu kwa mtu si kwamba kakosa kwa mungu ila ni wakati tuu ambao ni lazima apitie)×2
Usimuone mtu anapita kwenye jaribuu anavumilia kwa sababu ni wakati wake...maumivu aliyonayo hawezi mpa mtu ananyamaza kwa sababu ni kikombe chake...hakuna aliewahi omba kwa mungu apitie yale anayoyapitia, hakuna aliesema na mungu yampate yaleyale yanayompata...
(Jaribu lingeondolewa kwa kuomba sana wote tungeomba tusipite kwenye Jaribu, jaribu lingekwepeka kwa kufunga sana ndugu yangu wengi tungefunga tusipite kwenye jaribu...)×2
Mtu mwenye Jaribu hajaomba kwa mungu ni wakati tuu anapitia,Mtu mwenye pito hajaomba kwa mungu ni wakati tuu ni wakati anapitia...heee heee eeeeh
(Jaribu kwa mtu si kwamba ni mtenda dhambii...ila ni kikombe tuu lazima akinywe
Jaribu kwa mtu si kwamba kakosa kwa mungu ila ni wakati tuu ambao ni lazima apitie)×2
Instruments
Kulikuwa na Ayubu aliemcha Mungu..Mungu mwenyewe alijivunia Ayubu,
(Ayubu hakujua kwamba ipo siku moja itafika atapita kwenye jaribu)×2
Siku Moja Mungu akakutana na shetani akasema shetani wewe umetoka wapi.. shetani akajibu nimetoka duniani nikizunguka zunguka ah huku na kule, Mungu akasema Umemwona mtu wangu hapanaa mtu mwema kama ayubu...shetani akasema ni kwa sababu umemzingira pande zotee huyo...Jaribu kutoa kila kitu uone kama Ayubu hatakutenda dhambi,
Ayubu akaanza kupitishwa kwenye taabu yote kwa sababu mungu alijivunia ayubu,Ayubu akaanza kupitishwa kwenye mateso yote ni kwa sababu mungu alijivunia ayubu, Ayubu hakujua kwamba Mungu wa mbinguni anajivunia yeye, alipitia mengi, alisongwa na mengi, yote ni kwa sababu Mungu alijivunia Ayubu, alisongwa na mengii alipitia Mengi ,ayubu akasema pamoja na yote nitaishi eeeh eeeh
(Jaribu kwa mtu si kwamba ni mtenda dhambii...ila ni kikombe tuu lazima akinywe
Jaribu kwa mtu si kwamba kakosa kwa mungu ila ni wakati tuu ambao ni lazima apitie)×2
instruments
Ndipo nimejua kumbe yote yanipatayo mimi ni kwa muda, sijatenda dhambi, hujatenda dhambi, ni wakati tuu lazima tupitie, usimuone mtu analia sasa, ni mungu anajivunia hayo kumbe mengi yanatukuta sisi hatujui lakini mungu anajivunia sisi, anajua mwanzo anajua mwisho, ni baba anajivunia sisi unapitia mengii unasongwa na mengi kumbe mungu anajivunia wewe, tulia kwa mungu tulia kwa baba, ili mwenyewe ajitukuze kwako... kweli tunachoka kweli tunashindwa lakina Mungu anajivunia sisi...hatuwezi kuwa washindi hatuwezi kung'aa sana...lazima Mungu ajivunie hatuwezi kuendelea hatuwezi kuvuka ng'ambo lazima tupitie haya, JARIBU lako ni wakati tuu Mungu anajivunia, JARIBU lako ni wakati tuu ni wakati unapitia...eeeh eeeh
(Jaribu kwa mtu si kwamba ni mtenda dhambii...ila ni kikombe tuu lazima akinywe
Jaribu kwa mtu si kwamba kakosa kwa mungu ila ni wakati tuu ambao ni lazima apitie)×2
lyrics by Msafiri Njau