Asante Yesu Lyrics
- Genre:Afrobeats
- Year of Release:2009
Lyrics
Asante Yesu - Martha Mwaipaja
Asante bwana yesu kwa wema wako ulijitoa kwaajili
Yetu kama usingelikuwa wewe maisha yetu yangelikuwaje

Wewe umetangaza pumziko la kweli kwamba wote wenye
Mizigo waitue kwako kama sio wewe mwokozi kutupumzisha
Mizigo yetu tungeitua wapi
Tena umetanga kwa wenye magonjwa kwamba kwa kupigwa
Kwako wote wamepona kama usingejitoa kupigwa mtini
Wenye magonjwa wangeponywa na nani
Tena umesema na wote wenye kilio kwamba siku moja
Watanyamazishwa kama usingeyaona machozi ya wengi
Nani angeweza kujinyamazisha mwenyewe
Asante
Asante bwana yesu kwa wema wako ulijitoa kwaajili
Yetu kama usingelikuwa wewe maisha yetu yangelikuwaje
Asante bwana yesu kwa wema wako ulijitoa kwaajili
Yetu kama usingelikuwa wewe maisha yetu yangelikuwaje
Hata kwa walioshushwa chini wewe
Upo unamwinua mnyonge kutoka chini
Unakichagua kionekacho dhaifu ili
Upate kukiabisha chenye nguvu
Hata katika shida tunazopitia umesema yesu hautotuacha
Maana mkono wako si mfupi hata usiweze kututoa kwenye tabu
Ni kweli tunapita kwenye misukosuko lakini tunajua
Yesu wetu upo nasi maana umesema ni heri
Wenye huzuni siku yao ipo watafarijika
Asante bwana yesu kwa wema wako ulijitoa kwaajili
Yetu kama usingelikuwa wewe maisha yetu yangelikuwaje
Asante bwana yesu kwa wema wako ulijitoa kwaajili
Yetu kama usingelikuwa wewe maisha yetu yangelikuwaje
Hata kwa wasio na baba wewe upo umesema nikuite baba
Kama usingeuona ukiwa wangu ni nani leo ningemwita baba
Hata kwa mama yangu nimekuona umemvusha katika ujane wa
Tabu kwa misukosuko mingi aliyopitia bila wewe yesu asingeliweza
Wewe ni mungu utabaki kuwa mungu unatuwazia mawazo yaliyo mema ungekuwa
Mwingi wa ghadhabu kwa wanadamu ni nani leo hii angesimama