
Woga Wako Lyrics
- Genre:Afrobeats
- Year of Release:2011
Lyrics
Woga Wako - Rose Muhando
...
Woga wako ni ya umaskini wako mwanangu wueeh
hofu yako ndiyo kifo chako ye ye ye mama
mashaka nayo ni ya dhambi yako Yee mama wee
kila kitu nasema (huwezi)×3
kwani wengine wameweza vipii
malengo yako utafanikisha vipi eee
ndoto zako utakalimisha vipii
umejiroga mwenyewe
(epuka vikao vya wapumbavu eee)×2
acha kujifunza Kwa walioshindwa
walioshhindwa Wana maneno mengi
mchana kutwa utawaona vijiwe
wakijadili maisha ya wengine
wakiongelea mipango ya wengine
wakikosoa juhudi za wengine
flani ana gari ameongwa na flani
eti ana nyumba nzuri ameibia kampuni mama
lakini ya kwao yamewashinda
mchana kutwa wanashindana na jua
jua likisogea nao wanasogea
kivuli kikisogea nao wanasogea
hawajui kupambanua nyakati
mchana na usiku kwao ni sawasawa
eti mbona liende
CHORUS 1:
((pole)×4 umejiroga mwenyewe)×4
CHORUS 2:
(jeuri yako,,fedheha kwako, ujinga wako,upumbavu wako,fedhuli yako, ujinga wako hasira yako,hasara kwako,mpumbavu waamini kila neno jamani
nani mwenye akili hufiikiri Sana jinsii ya enda lavu)×2
CHORUS 1:
(Uchawi wa maisha yako ni wewe mwenyewe
adui wa mafanikio yako ni wewe mwenyewe
utagombana na watu bure
utawachukia wengine bure
utawakasirikia wengine bure
uchawi wa maisha yako ni wewe mwenyewe )×2
CHORUS 2:
CHORUS 1:
(Maneno ya mungu yanasema hivi)×2
Asiyefanya Kazi na asile
asiyefanya Kazi huyo ni mwizi
hafai katika jamiii yoyote jamani
wala hafai kwenye nyumba ya mungu
ni mchonganishi na mwenye fitina
mpita nyumba Hadi nyumba
mkorofisha ndugu Kwa ndugu
mgombanisha jamaa Kwa jamaa
asiyefanya Kazi ni mtu hatari
(nenda kajifunzee Kwa waliofanikiwa)×2
ebu waulize walifanya vipi
baada ya majibu chukua hatua mamas
Fanya Kazi Kwa mikono yako
utabarikiwaaa
mungu yupo
utafanikiwaaa
CHORUS 1:
(END)