
Ndivyo Ulivyo Lyrics
- Genre:Afrobeats
- Year of Release:2011
Lyrics
Ndivyo Ulivyo - Rose Muhando
...
Rose Muhando Naona kama maono, kumbe ndivyo ulivyo, Nilidhani 'kama ndoto, kumbe ndivyo ulivyo, Nilifikiri nachanganyikiwa kwa kusema hivi, kumbe ndivyo ulivyo, Umekuwa mpole, umekuwa mwenye huruma, kumbe ndivyo ulivyo ooh, Si mwepesi wa hasira, baba ni mwingi wa rehema, ndivyo ulivyo oh, Wewe unatuwazia mema, kuliko tunavyodhani, ndivyo ulivyo, Mawazo yako hayafanani na mawazo ya wanadamu, baba ndivyo ulivyo, Nani kama wewe, mwepesi wa kusamehe, ndivyo ulivyo ooh,
Jehova, Kumbe ndivyo ulivyo;
Ndivyo ulivyo, ndivyo ulivyo Ooh ndivyo ulivyo, Hakuna Kupinga. 2) Tulia kwa Mungu, hushuka na kutufariji, Baba kumbe ndivyo ulivyo oh, Usiku na mchana hulali husinzii Mungu uliye hai, ndivyo ulivyo ooh, Pale tusipoweza kutenda wenyewe kwa mikono yetu Yehova, ndivyo ulivyo ooh, Huingilia kati 'yale yote tunayoshindwa wewe ndivyo ulivyo, Msaada wakati tunapochoka, Yehova
Ndivyo ulivyo ooh;
3) Mungu uliwakusanya walioachwa, Ukawakumbatia baba ndivyo ulivyo, Waliokosa tumaini weka tumaini jipya kwao, ndivyo ulivyo ooh, Waliokata tamaa, wewe unawatia nguvu baba ndivyo ulivyo ooh, Vile nionavyo mimi si kama utazamavyo baba kumbe ndivyo ulivyo oh, Huruma zako zimevuka vilindi vya bahari, Mungu we eeh kumbe ndivyo ulivyo, Hakuna Kupinga;