Nipe Uvumilivu Lyrics
- Genre:Afrobeats
- Year of Release:2017
Lyrics
Nipe Uvumilivu - Rose Muhando
...
Nimekukimbilia wewe bwana Mwamba wangu na ngome yangu Nakuinulia macho yangu Baba mungu naja kwako Nainua mikono yangu juu Nahitaji msaada wako (repeat twice) Magonjwa mengi yamenitesa Yesu nipe uvumilivu Dhiki nyingi zimenisonga Baba nipe uvumilivu Watoto wangu wanaangaika Yesu nipe uvumilivu Walonizalisha wamenikimbia Baba nipe uvumilivu Maisha yangu yamo mashakani Baba nipe uvumilivu Baba, baba, Mungu nipe uvumilivu (Nipe bwana) baba, (bwana wangu) baba Mungu nipe uvumilivu Bwana, bwana, Yesu nipe uvumilivu Bwana, bwana, Yesu nipe uvumilivu Hata ndugu zangu wamenigeuka Nahitaji faraja yako Wamejitenga mbali nami Nasogea kitini pako Mbele yangu kuna giza kubwa Ndiwe mwanga wa njia zangu Wewe ni bwana, mume wa wajane Yesu nipe uvumilivu Tena wewe ni baba wa yatima Baba nipe uvumilivu Pia wewe ni mungu wa maskini Yesu nipe uvumilivu Baba, baba, Mungu nipe uvumilivu Baba, baba, Mungu nipe uvumilivu Bwana, bwana, Yesu nipe uvumilivu Bwana, bwana, Yesu nipe uvumilivu Adui zangu wamenizunguka Wataka kuniangamiza Wamenitegea mitego mingi Wanawinda roho yangu Nafsi yangu inazimia Njoo hima nisaidie (repeat twice) Baba, baba, Mungu nipe uvumilivu Baba, baba, Mungu nipe uvumilivu (Oh nakuhitaji Jehova Shama, Wewe umeketi mahali pa juu Wewe bwana wa wajane Wewe Mungu wa yatima Wewe unayeketi na maserafi na makerubi Wewe mungu wakati wa shida zangu Wewe uangazaye njia zangu Oh unipendaye nakimbilia kwako)