
Nipo Naye Lyrics
- Genre:Bongo Flava
- Year of Release:2021
Lyrics
Nipo Naye - Nandy
...
Asante baba kwa kuikata kiu yangu
Nimekutwa Shahidi nimeona ukuu wako
Imani haba umeitoa ndani yangu
Umekuwa mfariji (mfariji) tena mshauri wangu
Umerudisha tumaini langu wajua
Wanilinda kila nikipiga hatua
Tena umeondoa fedheha na mashaka yote
Pia umenitua mizigo hujaniacha mpweke
Hajaniacha nipo nae nipo na Yesu
baba nipo nae nipo na Yesu?
Naelewa fika Kuna kutabasamu na kulia
Mengi umeniepusha mengine hata sikutarajia
Pale nilipolia ulinifuta chozi na ukanishikilia
Umenitoa hatiani umenivika taji leo nafurahia
Tena umeondoa fedheha na mashaka yote
Pia umenitua mizigo hujaniacha mpweke
hajaniacha nipo nae nipo na Yesu
baba nipo nae nipo na Yesu?