![Una](https://source.boomplaymusic.com/group1/M01/87/AB/rBEeMVu_BCyAHMPaAAEOJ2MsZZU167.jpg)
Una Lyrics
- Genre:Bongo Flava
- Year of Release:2006
Lyrics
Una - Professor Jay
...
Una Sura nzuri na Tabia ya Kuvutia
Unaweza ukaishi popote katika hii Dunia
Una Tabasam pana la Hubba sauti nyororo
Kweli kwako nakiri umenifunga mi nyororo
Siwezi kuita hili libwata ataa
Mi nabisha kwenye hili suala mi nakataa
Una sura ya Mviringo Uzuri huna maringo
Na wallet imenenepa mithili ya Mama Pingo
Una Meno yalio Banana huna pengo wala Mwanya
Kidani cha ulimi mama nacho nichanganya
Una Macho madogo yasio hitaji miwani
Honey ki ukweli ukweli umenikamata Jamani
Una Shingo ya kuvaa Cheni nyembamba kiasi kwamba unatishia sana namba ya wote wanao Jigamba
Una Macho legevu utazani umevuta Wida ni kama Baba Ritha wada moja de wemafida
Una Chuchu kiduchu daima zanipa uchu
Simezi simungunyi nahema tu nusu nusu
Una lips kama umeficha Panya una nichanganya
Daima wewe ni wangu wa kufa na kuzikana
Una ngozi laini tena ya kungaaa
Una niuwa zaidi na hio Bamba taa
Una sifa zote ambazo mi nazipenda
Napenda tuwe wote kila sehemu ninayonkwenda
Naaziz masham sham kwako si mali huna habari Una ngozi kama ya nazi
Macho ya Kijapani kwako nishafika nafsi yangu imekita Kifuani chuchu saa sita
Machoni mtoto unanita
Binti umejaliwa busara uzuri na utashi
Una nakshi napenda harufu yako nzuri ya malashi Malkia wa moyo we pekee ndio Fahari ya Nafsi
Usiwe na wasi njoo sogea karibu young Dashh
Najiona niko mdotoni nadeka kama Utotoni mwengine kamwe sioni Nakupenda toka moyoni
Una jicho lako la bata Toto hujuwi kunata Mwanya kama Aminatha ndo mana mwenzio nadata
Una Tumbo dogo lenye mvuto sio kitambi Una Jua kumbembeleza kwa lugha isiyo na Kamandi
Mamy domo Kasuku na joto lenye hisia Dia una rangi ya mngaro na nuru isio fifia
Skia ujenzi wa mapenzi unakwenda ngazi kwa ngazi Niamini nikuamini ili tuyaepuke maradhi una
Una ngozi laini tena ya kungaaa
Una niuwa zaidi na hio Bamba taa
Una sifa zote ambazo mi nazipenda
Napenda tuwe wote kila sehemu ninayonkwenda
Una akili zaidi ya Linkon na unapenda kusoma Kwanza unatafakari kwa yote unayo yaona
Hutazami tu ya leo na unafikiri na kesho hata usipo elewa unaomba uwelewesho
Una kitovu cha kuweka pini mguu wa kimini umekaa sana akilini niamini Fukara mimi
Una miguu mithili chupa ya Bia aina ya Tusker heshima na Mapenzi ya kweli yasio na Maftaa
Ngozi laini utadhani Nacrach vocha midomo yako na ulimi huo ni uchawi tosha
Una nibamba sana kwa jinsi ulivyo Stebo Una thamani zaidi ya mpira Mweusi wa Poll Table
Mikono yako laini ya kushika Sim ndogo naisi utumbo wako haupitishi miogo
Hakika we ni wangu Tunzo maishani mwangu Daima unastahili kuwepo ubavuni mwangu
Una ngozi laini tena ya kungaaa
Una niuwa zaidi na hio Bamba taa
Una sifa zote ambazo mi nazipenda
Napenda tuwe wote kila sehemu ninayonkwenda
By: Yoram