![Jina Langu](https://source.boomplaymusic.com/group1/M01/21/4A/rBEezlu_GreAbjjaAAD_sot16uw198.jpg)
Jina Langu Lyrics
- Genre:Bongo Flava
- Year of Release:2001
Lyrics
Jina Langu - Professor Jay
...
Chorus;
Jina langu linavuma kwenye mitaa
Jina langu lina hadhi ya kisupa staa
Jina langu linaongeza idadi ya maadui
wengine nawajua wengine siwatambui
Jina langu..kwikwi eyo J tunakuzimia
Jina langu..J alosto ameshazeeka
Joseph Haule mc shupavu wa mitulinga
mchawi wa rhymes mti mkavu..
Verse 1;
Macho ya chinichini yanatizama nyendo zangu,
Najua hiyo yote sababu ya kipaji changu,
Sitaki kujua nani adui nani mwenzangu,
Na kwako muumba wangu ongeza hekima kwangu,
Hiyo sipo ukingoni miguu nje maji ya shingoni,
Mwenye tungo badili wamejizika shimoni,
Nani kabaki wapo kitaani mshumaa hauwaki,
Wameshindwa kuikabili fataki za itifaki,
Vina vyangu mahili kwenye giza kama kandili,
Na kwenye vichwa vya wapotevu naacha kitendawili,
Ni J mti mkavu niite nyota nyang'avu
Inayopigwa vita na wenye hoja chakavu,
Bado nachakarika na naona kaa za njoshi,
Eeh!! mola ni lini itakwisha hii mikosi,
Najuta kuitwa supa staa naona karaha,
Mangurubange na washikaji yananigasi nashangaa,
Huu ni mtafaruku na kero kwenye mitaa,
J njoo baba ni better tuvute raha,
Weka mapenzi kando nipeni hoja za msingi,
Wangapi mtanipenda nikiwa sina shilingi...
Chorus;
Jina langu linavuma kwenye mitaa
Jina langu lina hadhi ya kisupa staa
Jina langu linaongeza idadi ya maadui
wengine nawajua wengine siwatambui
Jina langu..kwikwi eyo J tunakuzimia
Jina langu..J alosto ameshazeeka
Joseph Haule mc shupavu wa mitulinga
mchawi wa rhymes mti mkavu..
Chorus 2;
Thamani ya ubongo wangu ni kubwa kuliko bingo,
Nashangaa mapromota bado mnaleta maringo,
Bado napiga goti kwa mungu aniongezee,
Kwenu vijana wa bongo poleni na starehe,
Jasho langu la chuma lataka moyo kulila,
Na wote mtabana ngenge wachawi na wenye hila,
Nimeshasebenza na shuluba nyingi za maisha,
Kumbukumbu tu ninazo mr ticha ..mr ticha,
Wape hi marekani wabongo mashabiki wa mbali,
Bongo dar es salaam mitego bado si shwari,
Ninapokosa hela washikaji wanatoweka,
Ninaporekebisha pumbavu wanasogea,
Naamini akili yangu ina akili kuliko mchwa,
Na ninajua hoja mpya ndo siku inapokucha,
Mwanga na saluti kumkoma nyani jirani,
Bado nipo makini siogopi mpinzani wa jadi,
Maneno yangu yajivu ni kama muarobaini,
Jamii inakubali vibwengo chomeni chini,
Wapo baadhi ya watu wanaotaka kunihukumu,
Wanatamani ningekuwa sioni waninyweshe sumu,
Wengi wananipenda wachache hamnipendi,
Skendo mnazonipa na mimi sipendi,
Mbio zipo ukingoni chomeka mbavu za mbwa,
Na chochote mnachosema bab kubwa...
Chorus;
Jina langu linavuma kwenye mitaa
Jina langu lina hadhi ya kisupa staa
Jina langu linaongeza idadi ya maadui
wengine nawajua wengine siwatambui
Jina langu..kwikwi eyo J tunakuzimia
Jina langu..J alosto ameshazeeka
Joseph Haule mc shupavu wa mitulinga
mchawi wa rhymes mti mkavu...
Verse 3;
J tunakuzimia at yahoo dot com,
Pande zote nitakwenda lakini bongo ndo hom,
Nazidi kuumiza kichwa nazidi kupata wafuasi,
Maisha ya starehe na ngono kwa sasa basi,
Nafungua milango kwa ajili ya kizazi kipya,
Na chance bado ipo wazi kwa wote waliojificha,
Kwenye matamasha nilidhulumiwa mshiko,
Mapromota walikimbia kabla ya kufanya malipo,
Sasa jino kwa jino nakwenda nao sambamba,
Napotembea haki siogopi nani katanda,
Leo nathibitisha ya kwamba kweli natisha,
Ni fukuto ulanjonjo kwa wote wanaobisha,
Fukara wa kipato nina akili za kitajiri,
Na muda utakapozidi naamini wote mtakiri,
HBC muongozo wa ma-mc kamati kuu ya wanga imebi...
Chorus;
Jina langu linavuma kwenye mitaa
Jina langu lina hadhi ya kisupa staa
Jina langu linaongeza idadi ya maadui
wengine nawajua wengine siwatambui
Jina langu..kwikwi eyo J tunakuzimia
Jina langu..J alosto ameshazeeka
Joseph Haule mc shupavu wa mitulinga
mchawi wa rhymes mti mkavu..