![Hapo Sawa](https://source.boomplaymusic.com/group2/M01/25/2C/rBEeqFu_DhqAGMUfAAFYEukO3kU759.jpg)
Hapo Sawa Lyrics
- Genre:Bongo Flava
- Year of Release:2008
Lyrics
Hapo Sawa - Professor Jay
...
chorus***
kindagarten mpaka chuo kikuu,
downtown Kwa machizi na ma sister duu mikono juu,
hapo vipi (hapo sawa) ×2
magharibi mpaka za nyanda za juu,
Kanda ya ziwa kaskazini mpaka east zoo I'm coming through
hapo vipi hapo sawa ×2
verse 1
*********
hapa kati chembe kidevu lazima ukae,
nachana zaidi ya wembe kama mwelevu usinishangae,
Mimi sio kiongozi napigania ukombozi ,
nakaba kooni zaidi ya jinamizi kwenye njozi,
nasaka haki sio kilio Cha samaki,
machozi kwenda na maji
hiki kipaji sio bahati (ndio),
akili yangu sio uwanja wa majaribio neno langu linaongeza faraja kwenye vilio,
nafikiri nifike sisemi tu nisikike,
jasho langu linafanya malengo niyafanikishe,
Niko tayari Kwa kheri ama Kwa shari,
jino Kwa jino ukimwaga mboga namwaga ugali,
maisha yenyewe kamari hatari ndani ya safari,
kichwani vina kama mchanga wa bahari,
huu ni muhimili wangapi mnawabashiri,
na kuwavisha Mataji Kwa vina vya tafsiri
*** chorus***
kindergarten mpaka chuo kikuu,
downtown Kwa machizi na ma sister duu mikono juu,
hapo vipi (hapo sawa) ×2
magharibi mpaka za nyanda za juu,
Kanda ya ziwa kaskazini mpaka east zoo I'm coming through
hapo vipi hapo sawa ×2
**** verse 2***
ili nifanikiwe nahitaji marafiki,ili nifanikiwe zaidi nahitaji maadui,
mkononi Sina tattoo bali nna alama ya ndui,
mtanzania namba Moja majungu hayasumbui,
mchaka mchaka nakimbiza Kila upande,
simtumikii kafiri ili chati yangu ipande,
get off my shoulder ngoma inavuka boarder,
muda unazungumza wa mia hapati Moja,
pori Kwa ford hata vipi imebaki story,
kama zama za mtikila na sera za gabachori,
naishi biashara daima siogipi hasara,
na mara Kwa mara hii busara huepusha madhara,
napoza Nile kama nahisi Cha moto,
napokea matatizo yangu kama changamoto,
nipo ili nife nanena bila kificho,
naitunza heshima yangu zaidi ya mboni ya hicho
*chorus****
kindergarten mpaka chuo kikuu,
downtown Kwa machizi na ma sister duu mikono juu,
(hapo vipi hapo sawa) ×4
magharibi mpaka za nyanda za juu,
Kanda ya ziwa kaskazini mpaka east zoo I'm coming through
(hapo vipi hapo sawa) ×4
****verse 3****
wewe Bora mwanamziki Mimi mwanamuziki Bora,
chart zetu hazifanani kama mafua na ebora,
mwenye hekima huona haja na kujificha,
Bali mpumbavu huende mbele na kuvimba kichwa,
nani anabisha simama kuthibitisha ,
niite mwanaharakati hip hop naiwakilisha,
Fanya ufanyavyo akili yangu haikwepeki
unataka kua dj copy kama double deck,
siui mende Kwa nyundo mana nitaumia Mimi,
na ndio mana nawadharau mnaotaka bifu na Mimi,
born town kitambo utanieleza Nini
wakati huo wengi wenu hata hamjakuja mjini
.......,.....................
chorus*****
kindergarten mpaka chuo kikuu,
downtown Kwa machizi na ma sister duu mikono juu,
(hapo vipi hapo sawa) ×4
magharibi mpaka za nyanda za juu,
Kanda ya ziwa kaskazini mpaka east zoo I'm coming through
(hapo vipi hapo sawa) ×4
kindergarten mpaka chuo kikuu,
downtown Kwa machizi na ma sister duu mikono juu,
(hapo vipi hapo sawa) ×4
magharibi mpaka za nyanda za juu,
Kanda ya ziwa kaskazini mpaka east zoo I'm coming through
(hapo vipi hapo sawa) ×4
lyrics by @dennyka1 ( insta )